Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mbunge wa Jimbo la Gairo Ahmed Shabiby akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2024/25 Bungeni Jijini Dodoma leo May 23,2024 ameiomba Wizara hiyo kupitia Bodi ya Filamu Tanzania kuziangalia upya Filamu zenye maudhui ya ushirikina (kichawi) akidai kuwa zinaharibu na kuharibu fikra za Watanzania.
“Mnajua mnawaharibu Watu kisaikolojia Watu wengi wanaharibika kisaikolojia hapa Tanzania ni kwa ajili ya vitu kama hivi vya hovyo unaweza ukamkuta Mtu anashinda kwa Mganga ameona kwenye Filamu kuwa kumbe uchawi upo na Mtu anafanikiwa ukienda.
Watoto wadogo nao wanaharibika na hawa Watoto wanaoangalia Filamu mjue mnaandaa Waganga na Wachawi wa baadaye ndio maana Watanzania wengi wanashinda kwenye mitandao hawafanyi kazi yoyote wanakuwa Wambeya kwasababu hakuna vitu vya maana ambavyo vinawafundisha”.
Mnakubaliana na hoja hii wakuu?