Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. CONDESTER SICHALWE AFANYA MKUTANO NA WAKULIMA WA KIJIJI CHA NKALA, MOMBA
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe, Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe na Afisa Kilimo wamekutana na wakulima wa Kijiji cha Nkala na kuwasisitiza kuhudhuria mafunzo ya Kilimo yanayotolewa na Maafisa Kilimo.
Katika Mkutano huo wa hadhara, Mhe. Condester Sichalwe aliambatana na Maafisa Kilimo wa Kijiji cha Nkala ambao walizungumza na wananchi kuhusu Kilimo chenye tija, Mbegu bora za kutumia na jiografia ya eneo inayoendana na aina ya Kilimo cha Mpunga
Wananchi wa Kijiji cha Nkala wametoa maoni yao kuhusu mwenendo wa Sekta ya Kilimo huku wakidai kukutana na changamoto za Kukosa mikopo, kupewa mbegu ambazo hazifai, kukosa mbolea na wananchi wa chini Kukosa mikopo wanapoomba, wazee wa TASAF kutopata stahiki zao na kutokuwa na benki Nkala ili fedha wazichukulie hapo hapo Kijijini
Mhe. Condester Sichalwe amesema kuwa wananchi wanapaswa kuunda vikundi vya ushirika ili waaminike kupewa mikopo kwani wananchi wengine dhamana yao ni vikundi vya pamoja.
Mhe. Condester Sichalwe amesema ili ulime na upate faida nzuri ni lazima kuzingatia ubora wa udongo, ubora wa mbegu, jiografia ya eneo na kuomba Wataalam wa TASAF kukutana na wahusika ili kushauriana na wazee kwanini TASAF zao zinachelewa sana.