PreGE2025 Mbunge Sophia Mwakagenda aitema CHADEMA, Ajiunga rasmi na CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Duh, ubinafsi na njaa itawamaliza Hawa. SAWA Kwa kuwa tangu mwanzo hapo wabunge hao si wa zizi la Chadema.
 
Huyu Alifukuzwa Chadema pamoja na Halima Mdee na wenzake

View attachment 3320168

Hata hivyo hatoondolewa Bungeni na atalipwa hela za umma zote za mafao
Huyu alishatimuliwa Chadema siku nyingi, hana chama, ni kielelezo chauvunjaji wa Katiba ya nchi kwani sifa kubwa ya kuwa mbunge ni kuwa mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa.
 
Aende tu, kutumikia wananchi atakuwa yeye? Tunajua focus ni tumbo na siyo wananchi aache kudanganya umma
 
Huyu Alifukuzwa Chadema pamoja na Halima Mdee na wenzake

View attachment 3320168

Hata hivyo hatoondolewa Bungeni na atalipwa hela za umma zote za mafao
Kwani huyo na wenzie 19 si walishafukuzwa chamani? Kuhamia huko haiwezi kuwa habari ya kushtukiza maana ni mwanasiasa so lazima atafute platform ya kufanyia ujinga (siasa) wake na kaona aelekee kwa waliomtuma.
 
Hivi huwa wanatumikia wananchi siku gani?
Kila mmoja anasema anaenda kuwatumikia wananchi zaidi 😄
 
Alichelewa mbona hanafaida Kwa chadema,aende akijua CCM inawenyewe
 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda, ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), akisema uamuzi huo unalenga kuendeleza jitihada zake za kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bulyaga iliyopo Tukuyu, mkoani Mbeya, ametumia nafasi yake kuwaaga wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akikipongeza kwa kumlea na kumjenga kisiasa tangu aanze safari yake ya uongozi.

“Ninashukuru CHADEMA kwa malezi na mafunzo ya kisiasa niliyoyapata, kuanzia saa tano asubuhi ya Juni 28, 2025, nitajiunga rasmi na CCM ili kuendelea kuhudumia wananchi,” amesema Sophia.

Hata hivyo, Mwakagenda bado hajafichua kama atawania Ubunge wa Jimbo la Rungwe katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Mwakagenda ni miongoni mwa wabunge 19 wa Viti Maalum waliovuliwa uanachama na CHADEMA. Katika uchaguzi wa mwaka 2020, aliwania Ubunge wa Jimbo la Rungwe kupitia tiketi ya CHADEMA, akichuana na mbunge wa sasa, Antony Mwantona wa Chama cha Mapinduzi (CCM)


Cc Nipashe
 
Huyu si alishafukuzwa chadema?
 
Chadema haina mbunge viti maalumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…