Mbunge Sospeter Muhongo ameniogopesha kwa kauli yake kuhusu ujenzi wa bwawa la Rufiji; je, kuna haja ya wabunge wote kupimwa akili?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Tangu niliposikia kauli ya Mbunge Sospiere Mukweli akisema kwamba ujenzi wa mabwawa ya kufua umeme kwa sasa yamepitwa na wakati, akili yangu imevurugika kabisa nisielewe nini kinaendelea kichwani mwa wabunge wetu, nimeogopa sana.

Na hii imekuja baada ya ile kauli ya hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli ya kwamba mtu anayeweza kukubali masharti ya mkataba wa Bandari ya Bagamoyo ni mlevi tu (aliyechanganyikiwa) kudhihirika kwa mbunge Kazi Ndugu gay; nimetetemeka sana.

Kuhusu suala la mabwawa ya kufua umeme kuwa yamepitwa na wakati, niseme tu out right, bila uwoga wala aibu, ni uwendawazimu, hakuna sane person katika hii dunia, let alone a professor, anaweza kutoa ile kauli, nawahakikishia, zungukeni hii dunia yote, hakuna binadamu mwingine hata mmoja anaweza kukubaliana na hiyo kauli, nitaeleza kwanini.

1) Dunia kwa sasa inapambana kwa nguvu zote na tatizo la ‘Global warming’, katika vita hii, mbinu kubwa inayotumika ni kupunguza matumizi ya nishati zinazozalisha hewa ya ukaa (fossil fuels), na badala yake wanahimiza matumizi ya ‘renewable energy sources’ ambazo ni ‘sustainable’ na hazizalishi hewa za ukaa (greenhouse gases) na hivyo kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Renewable sources zinazohimizwa ni kama Nishati ya upepo ‘Wind turbines/mills), Nishati joto (Geothermal), Nishati jua (Solar energy) nk; lakini kubwa na yenye uhakika zaidi ni umeme wa nguvu ya maji (Hydroelectric power/ HEP) kama hii tunayojenga sisi.

Na ndio maana ifikapo mwaka 2030, nchi nyingi hasa za ulaya, zimepanga kupiga marufuku magari yanayotumia ‘fossil fuels’ na badala yake wataruhusu gari za umeme tu. Sasa mniambie, with all due respect, na sina nia ya kumvunjia mtu heshima, hivi, mtu anaesema umeme wa nguvu ya maji umepitwa na wakati, yuko sawa katika utimamu kamilifu wa fahamu zake?!

2.) Nchi zote zinazokua kiuchumi zinategemea viwanda imara vyenye ufanisi na tija katika uzalishaji kiasi viweze kushindana katika soko la ndani na soko la kimataifa. Pia inafahamika, nishati ya uhakika na ya bei nafuu ndio kiungo muhimu katika kufanikisha uimara na ufanisi wa viwanda vyenye tija ya uzalishaji. Katika vyanzo vya umeme salama na vyenye gharama nafuu zaidi katika uzalishaji ni umeme utokanao na nguvu ya maji, hata taahira anaekota makopo majalalani anaujua ukweli huu, sembuse Profesa?!

Hivyo basi, kwa kauli mbiu ile ile ya Hayati Rais John Joseph Pombe Magufuli ya uchumi imara utajengwa na viwanda (Tanzania ya viwanda),na wote tunafahamu ile multiplier effect ya uwepo wa viwanda, kuanzia ajira, ukusanyaji kodi nk; sasa sioni ni namna gani mtu mwenye ukamilifu wote katika fahamu zake, anaweza kusema kwamba uzalishaji umeme kwa mabwawa umepitwa na wakati, no way!

3) Mabwawa ya kufua umeme huwa hayatumiki kwa ajili ya kufua umeme tu pekee yake, haya mabwawa hutoa chanzo cha uhakika cha maji kwa ajili ya shughuli mbalimbali kwa ajili ya kilimo na matumizi mengine ya binadamu na mifugo, ambapo bila uwepo wa bwawa, hayo maji yangemwagikia tu baharini huku wanachi wakibaki na uhaba wa maji bila sababu ya msingi, na wote tunajua multiplier effect itokanayo na kilimo cha uhakika (irrigation) tofauti na kilimo cha kubahatisha mvua. Hivyo mabwawa ya kufua umeme hayawezi kuwa yanepitwa na wakati, no way!!!

Naoendekeza huyo Profesa aende bungeni kwa magoti na kuomba msamaha kwa kauli yake ya kinafiki, na aeleze, ni kwanini amefanya vile??! Kitu kibaya sana amefanya huyu mzee, WaTanzania kwanini mnamkalia kimya huyu mtu, ashikiwe bango akaombe msamaha!

Na bado Bwana Kazi Ndugu gai...

Sasa je, kuna umuhimu wa kidharura wa kuwapima akili wabunge wote?!

=================================
Update: 12/12/2021
- Inaumiza sana kuona mradi wa bwawa la Nyerere unahujumiwa wazi wazi


PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA
 
Haya yote Ni kutuaminisha kuwa MJOMBA hakufanya jambo zuri katika Taifa hili

MJOMBA tunampenda na hakuna nyau yeti atakae futa mhuri wake katika mioyo yetu.
Sema Unampenda.Kongosho wewe.!
 
Haya yote Ni kutuaminisha kuwa MJOMBA hakufanya jambo zuri katika Taifa hili

MJOMBA tunampenda na hakuna nyau yeti atakae futa mhuri wake katika mioyo yetu.
Wakati wa uhai wake tuliambiwa badala ya kusema "hatuna pesa, hali ni ngumu" sema "sina pesa, hali ni ngumu.' Ikiwa na maana ya kutaka kila mmoja aisemee nafsi yake. Nadhani tunaelewana.
 
Wakati wa uhai wake tuliambiwa badala ya kusema "hatuna pesa, hali ni ngumu" sema "sina pesa, hali ni ngumu.' Ikiwa na maana ya kutaka kila mmoja aisemee nafsi yake. Nadhani tunaelewana.
Anasemea nafsi za wote wenye mtizamo sawa na wake, hivyo inabidi atumie ‘wingi’
 
Kwakweli Muhongo anatukosea, yeye aidha ni mdau au anajua atafaidika na makampuni ya nje ambayo yanazalisha gas na umeme wa gas wanaouzia tanesco.

Makampuni haya yanapata faida kubwa sana kutoka watanzania wa kawaida wanaotumia umeme. Nadhani mikataba yao ilishaongelewa sana wakati akiwa waziri....

Ikiwa umeme wa maji haufai, mbona Ethiopia wanabwawa lao nadhani ndio kubwa kuliko yote Africa la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) limeanza kujengwa 2011 mpaka sasa halijakamilika. Bwawa hili la umeme linatishia vita kati ya Misri na Ethiopia baada ya kutofikia namna ya ujazwaji wake kutumia maji ya mto Nile. Hili bwawa litazalisha umeme wa giga watss 6.3 mara 3 ya bwawa la Rufiji/Nyerere.

Kwahiyo si kweli kuwa umeme wa maji haupo bafo upo sana tu.

 
dalali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…