Pre GE2025 Mbunge Sylvia Sigula azindua Kituo cha Mafunzo ya Ushonaji, Urembo, Mapambo na Ujasiriamali kwa Vijana wa Mkoa wa Rukwa

Pre GE2025 Mbunge Sylvia Sigula azindua Kituo cha Mafunzo ya Ushonaji, Urembo, Mapambo na Ujasiriamali kwa Vijana wa Mkoa wa Rukwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Mbunge wa Viti Maalum Sylvia Sigula amezindua kituo cha mafunzo ya ushonaji, urembo, mapambo na ujasiliamali kwa Vijana wa Mkoa wa Rukwa lengo likiwa ni kutoa mafunzo na vitendea kazi kwa Vijana ili waweze kujiajiri ili kupunguza changamoto ya Ajira, kituo hicho kipo chini ya Taasisi ya Sigula Wezesha Fundation ambayo Mkurugenzi wake ni Mbunge huyo.

Kituo kimesajiri Vijana 42 katika awamu ya kwanza ambao watapatiwa mafunzo na Walimu wenye ujuzi na uzoefu mkubwa kwenye masuala la ushonaji, urembo, mapambo, kutengeneza batiki na ujasiriamali ndani ya miezi mitatu bila Wanafunzi kulipa chochote yani bure kabisa na wakihitimu watapewa cherehani bure kila mmoja ili wajiajiri na kujiongezea kipato.

Jambo hilo limeungwa mkono na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye amechangia Tsh. 300,000 kwa ajili ya ununuzi wa vitambaa vya kujifunzia huku Mbungr wa Jimho la Sumbawanga mjini Aesh Hilary akiunga mkono wazo hilo na kuchangia Tsh. 2,000,000 kwaajili ya ununuzi wa computer ili ofisi iwe ya kisasa na kuwasaidia Vijana kuwa Wabunifu zaidi katika kazi zao na pia amechangia cherehani 10 zenye thamani ya Tsh. 3,000,000 ili kuongeza uwezo wa Taasisi hii kuongeza usajili wa Vijana kwakuwa uhitaji ni mkubwa ukilinganisha na uwezo wa Taasisi.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sylvia Sigula amesema dhamira ya Taasisi hio ni kuona kila Kijana anachangamkia fursa na kutokubaki nyuma kwenye suala la kujikwamua kiuchumi.

 
Back
Top Bottom