Mbunge Sylvia Sigula: Mifuko ya Mikopo ya Serikali Haijafika kwa Walengwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNE SYLVIA SIGULA: MIFUKO YA MIKOPO YA SERIKALI HAIJAFIKA KWA WALENGWA​

Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Sylvia Sigula amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika kuanzisha mifuko mbalimbali ya kutoa mikopo, lakini asilimia kubwa ya mikopo hiyo haifiki kwa walengwa na asilimia kubwa ya watu hawana ufahamu wa kutosha kuhusu mikopo inayotolewa na Serikali kwa makundi maalumu likiwemo la vijana.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11, 2025 bungeni Dodoma, Mhe. Sylvia Sigula amesema mikopo ambayo inafahamika kwa kiasi kikubwa ni ile ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri, lakini kuna mikopo mingine zaidi ya hiyo ambayo bado watu hawaifahamu ikiwemo
mifuko zaidi ya 20 ambayo inatoa mikopo moja kwa moja kwa walengwa, mifuko 26 inayotoa ruzuku chini ya Serikali, progamu tisa za uwezeshaji wananchi kiuchumi na nyinginezo.

Hivyo, Mhe. Sylvia Sigula ameishauri Serikali kuja na mkakati maalumu wa kutoa taarifa kwa vijana kuhusu mikopo hiyo na kuunganisha mikopo hiyo pamoja na ile ya halmashauri ili kama kijana akikosa mikopo hiyo kwa sababu mbalimbali basi halmashauri imuunganishe moja kwa moja na mikopo mingine aliyoitaja.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-04-12 at 06.09.14.mp4
    24.6 MB
CCM ni kirusi inawapa vijana pikipiki masharti lazima uww na Kadi ya CCM na uhurudhurie vikao vya chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…