Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Sylvia Francis Sigula ameihoji Serikali ni magari mangapi ya Serikali yamefungwa mfumo wa gesi baada ya kuanza kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo huo.
Sigula amehoji hilo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Makadiro ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa Fedha 2024/25.
“Tumeona kwenye hotuba zaidi ya magari 3000 yamebadilishwa kwenye mfumo wa gesi lakini tunasema Watanzania wanatamani kuendelea kutumia gesi kwenye magari yao kwasababu ni gharama nafuu na tumeona mna mpango wa kuongeza vituo japo ni vichache lakini vifaa vya kubadilishia mifumo ni gharama sana ukitaka kubadili sio chini ya milioni mbili lakini sijaona Serikali ambayo ndio inasimamia jambo hili hamasa ipi inatupa Serikali wao kama Serikali ni magari mangapi yamefunga gesi?