Mbunge Tabasamu: Kuna uhaba wa walimu lakini hamtaki kuajiri

Mbunge Tabasamu: Kuna uhaba wa walimu lakini hamtaki kuajiri

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge wa Jimbo la Sengerema (CCM), Hamis Hussein Tabasamu, amesema licha ya uwepo wa upungufu wa walimu na waliosomea kuwepo mitaani, Serikali imekuwa haitoi Ajira

Amesema, "Mimi nafikiri Mtaala wa Ualimu ufutwe katika Vyuo Vikuu kwasababu watu wanapelekwa kusomea Ualimu lakini wanaendelea kuwepo mitaani

Ameongeza, "Watu wanaenda kusomea Ualimu, una upungufu hautaki kuajiri. Hawa Vijana wetu itakuwaje? Upungufu tunao, lakini hamtaki kuajiri mnakuja na Ajira 6,000. Mimi nashindwa kuelewa hilo jambo"
 
Pia pale Sengerema hospital hakuna huduma nzuri wala dawa hakuna asisahau hilo
 
Yule ni mmiliki wa shule , ana shule zake , ni mdau wa Elimu Sana , hii serikali ya kijiwe jiwe inawaza madege tu. Ndo mana tunatofautiana kwenye kifo cha Magufuli , wengine wanaskitika wengine watafurah tu.
 
Asisahau pia vijana tunapewa mafunzo ya kijeshi JKT halafu tunarudi uraiani.
 
Nilimfahamu sana enzi nachukua mabondo visiwa vya sengerema na kupeleka kwa wachina Uganda, naona biashara yenyewe ya mabondo sijui ikoje siku hizi, kule nilienda kusaka maisha ndio nikamfahamu.
Hongera sana mjasiliamali.
Kwani biashara imesimam?
 
Asisahau pia vijana tunapewa mafunzo ya kijeshi JKT halafu tunarudi uraiani.
China, Korea Kaskazini na kusini kuna umri ambao kila mtu ni compulsory kwenda jeshi kwa mwaka mzima kisha wanarudi uraiani
 
Mbunge wa Jimbo la Sengerema (CCM), Hamis Hussein Tabasamu, amesema licha ya uwepo wa upungufu wa walimu na waliosomea kuwepo mitaani, Serikali imekuwa haitoi Ajira...
Mmmghhhh
 
Tunamkumbusha barabara za mitaani sengerema hazitengenezwi. kwa miaka kadhaa sasa wengine wameamua kulima katikati ya barabara hizo hali inayo leta usumbufu unapo hitaji huduma ya gari hususani mitaa ya kilabela, ibisabageni na mnadani
 
Jamaa ana point sana,

ukosefu wa ajila kwa vijana wetu Ni disaster kubwa sana.

Afu Kuna jitu limepita uko kihuni bila kupingwa, linakuja kusema eti vijana wajiajiri.

Hivi mtu aliesomea ualimu anajiajili vipi Kama ata twisheni mitaani nazo mmezipiga marufuku.
 
Mh Rais SSH karuhusu ajira 6,000 za walimu. Labda kama ninaota mnisahahishe.
 
China, Korea Kaskazini na kusini kuna umri ambao kila mtu ni compulsory kwenda jeshi kwa mwaka mzima kisha wanarudi uraiani
Uchumi wa China na Korea unaulinganisha na wa Tz,sidhani kama unemployment rate ya China iko sawa na ya Tanzania.
 
Tunamkumbusha barabara za mitaani sengerema hazitengenezwi. kwa miaka kadhaa sasa wengine wameamua kulima katikati ya barabara hizo hali inayo leta usumbufu unapo hitaji huduma ya gari hususani mitaa ya kilabela, ibisabageni na mnadani
Kwa kweli Ngeleja sijui aliwahi kulifanyia nini hilo jimbo.
 
Mh Rais SSH karuhusu ajira 6,000 za walimu. Labda kama ninaota mnisahahishe.

Hizo sio ajira isipokua kuna idadi ya walimu 6000 waliostaafu, waliokufa na walioacha ajira hivo hiyo ni replacement ya kawaida. Mahitaji ya walimu ni makubwa shule nyingi hazina walimu mfano geita huko shule ina watoto karibu 600 darasa la kwanza hadi la saba na kuna walimu wawili tu, sijui umeelewa au bado?
 
Back
Top Bottom