Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo amesema serikali haipaswi kulaumiwa kwa ukosefu wa haki kwenye vyombo vya sheria, bali lawama ziende kwa watendaji kwani sheria zipo wazi.
Akichangia hoja ya Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Sheria Ndogo, Tadayo amesisitiza kuwa hakuna sababu ya mtu kunyimwa dhamana kwa kosa linalostahili dhamana.
"Ikikosekana haki tusilaumu serikali wala sheria, tulaumu watendaji kwa sababu sheria zipo na zinatoa kila fursa," amesema Tadayo.
Ameishauri serikali kuendelea kuwekeza katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mtu.