Pre GE2025 Mbunge Tauhida Gallos Akabidhi Vifaa vya Ujenzi Ofisi za CCM Jimbo la Dimani, Magharibi - Zanzibar

Pre GE2025 Mbunge Tauhida Gallos Akabidhi Vifaa vya Ujenzi Ofisi za CCM Jimbo la Dimani, Magharibi - Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.36.jpeg

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Magharibi (Zanzibar), Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo katika ziara aliyofanya tarehe 09 Oktoba, 2024 Jimbo la Dimani ameahidi kushirikiana na Viongozi wengine katika kutatua matatizo mbalimbali ya Wananchi.

Akikabidhi Mchanga na Mifuko ya Saruji kwa Viongozi wa CCM Katika Jimbo la Dimani, Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo amesema ametoa vifaa vya ujenzi ili kusaidia kufanya matengenezo ya Ofisi ya CCM ili kuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa ufanisi.

Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo katika hotuba yake ameahidi kuendelea kushirikiana na Viongozi wa Jimbo la Dimani katika kuwaletea maendeleo Wananchi na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, Mbunge Tauhida Gallos Nyimbo Amewataka viongozi kufanya kazi kwa bidii na kuachana na majungu, fitina na uhasama jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani, Ndugu Rehema Haji Makame amesema maendeleo hayo yameweza kupatikana kutokana na mashirikiano yaliyopo baina ya Wananchi, Serikali na Chama Cha Mapinduzi. Amewataka kushirikiana katika kudumisha suala la amani na utulivu iliyopo nchini ili Viongozi waendelee kuwaletaea maendelao Wananchi.

WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.54(1).jpeg

Naye, Mbunge wa Jimbo la Dimani, Mhe. Mustafa Mwinyi Kondo amempongeza Mbunge Mhe. Tauhida Gallos Nyimbo kwa juhudi kubwa anazozichukuwa katika kuwatumikia UWT, Chama Cha Mapinduzi na Wananchi kwa ujumla.

Hivyo, Mhe. Mustafa Mwinyi Kondo ameahidi kushirikiana na kuwa kitu kimoja ili kuweza kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.53.jpeg

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.52(3).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.52(3).jpeg
    117.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.52(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.52(2).jpeg
    138.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.49(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.49(2).jpeg
    78.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.49.jpeg
    67.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.34(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.34(2).jpeg
    102.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.48.jpeg
    141.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.44.jpeg
    WhatsApp Image 2024-10-09 at 16.31.44.jpeg
    104.3 KB · Views: 5
Back
Top Bottom