MBUNGE TAUHIDA GALLOS: Kliniki ya Kutatua Migogoro ya Ardhi Iwe Endelevu Kila Mkoa, Jimbo na Wilaya

MBUNGE TAUHIDA GALLOS: Kliniki ya Kutatua Migogoro ya Ardhi Iwe Endelevu Kila Mkoa, Jimbo na Wilaya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MBUNGE TAUHIDA GALLOS: Kliniki ya Kutatua Migogoro ya Ardhi Iwe Endelevu Kila Mkoa, Jimbo na Wilaya

MHE. TAUHIDA GALLOS, Mbunge wa Viti Maalum Akichangia Hotuba ya Bajeti Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Katika Mwaka Mpya wa Fedha 2024/2025

"Nampongeza Waziri na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwatumikia watanzania. Maneno ninayokupa kama zawadi nenda kasome kitabu cha 1 Wafalme. 3:16-24 kaangalie Hekima za Suleiman. Mungu amekupa zawadi ya hekima, ni vitu ambavyo viongozi tunapswa kuwanavyo" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum

"Watendee haki watanzania, mfikirie mtanzania aliyekuwa mnyonge kila alipokuwa anaenda kwenye Mahakama kuitafuta haki alikuwa anaikosa. Wewe Waziri ukawe mkombozi wake. Watanzania wamenituma wanasema nikuombe ile Kliniki ya Ardhi iendelee" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum

"Kuna watu wanatoka Zanzibar ambao walioa na kuolewa ila walidhurumiwa ardhi zao wakati wazee wao wanaoishi Tanzania Bara walipofariki. Leo kupitia Kliniki ya Ardhi wanakuja kutafuta haki zao. Waziri naomba tafuta muzunguko endelevu kwa kila Mkoa, Jimbo na Wilaya. Kliniki ya Ardhi ni majibu tosha ya watanzania" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum

"Mipango mizuri ya Ardhi na matumizi mazuri ya Ardhi ni kitu kitakachoenda kuondosha migogoro ya Ardhi ndani ya Tanzania. Lazima Wizara zikubali kushirikiana ikiwemo TAMISEMI, Kilimo na Mifugo. Wekeni mipango mizuri itakayoenda kumkomboa Mtanzania" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo, Mbunge wa Viti Maalum

"Mfumo wa vijiji vyetu jinsi vilivyo hata maendeleo kwenda kwao yanakawia. Kijiji kimoja kipo huku na Kijiji kingine kipo kule, kufikiwa na miundombinu inakuwa kazi ngumu, tunajipa mzigo mkubwa watanzania kwasababu hatujipangi vizuri

"Waziri wa Ardhi imarisha kitengo chako cha utoaji wa Hati na ukipe nguvu. Kama hakina fedha kipelekee fedha, magari na kompyuta. Migogoro mikubwa kwa watanzania ni pamoja na kutokupata hati kwa wakati. Muda anaokawizwa kupata hati tangu amemiliki kiwanja ndicho kinapelekea madalali na makanjanja wanatumika ngani ya Wizara ya Ardhi ndipo wanabadilisha matumizi ya Ardhi kwenda kwa mtu mwingine"

 
Back
Top Bottom