Mbunge Twaha Mpembenwe: Force Account Idhibitiwe Katika Kutekeleza Miradi

Mbunge Twaha Mpembenwe: Force Account Idhibitiwe Katika Kutekeleza Miradi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Mbunge Twaha Mpembenwe: Force Account Idhibitiwe Katika Kutekeleza Miradi

WABUNGE wametilia shaka matumizi ya Force Account katika kutekeleza baadhi ya miradi ya Serikali.

Wawakilishi hao wa wananchi wameonesha wasiwasi wao huo wakati wa mjadala wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) bungeni mjini Dodoma.

Baadhi yao wameshauri utaratibu huo udhibitiwe kwa kuwa umeonekana kuwa na mapungufu mengi yanayosababisha matumizi mabaya ya fedha za umma.

Kati ya wabunge waliochangia hoja hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Twaha Mpembenwe ambaye amesema Serikali inapaswa kuchanganua na kuweka tafsiri sahihi ya aina ya miradi ya kutekelezwa kwa utaratibu wa Force Account.

Amesema hiyo ni kwa sababu miradi midogo haileweki ni miradi ya namna gani na ndio sababu utaratibu wa Force Account unatumika pia kwa miradi yenye thamani kubwa.

Ameongeza kuwa wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ikikagua miradi imekutana na miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 5 hadi 6 ambayo imetekelezwa kwa kutumia Force Account na ndipo akahoji: “Je, hiyo ndio miradi midogo au mikubwa?”

Ni katika muktadha huo, amesema ni wakati mwafaka sasa kwa Serikali kufanya tathmini kama madhumuni ya kuanzishwa kwa Force Account yanaleta tija au la
 

Attachments

  • FdW30K8a_400x400.jpg
    FdW30K8a_400x400.jpg
    24.4 KB · Views: 5
  • GGX4j03WYAAUc_K.jpg
    GGX4j03WYAAUc_K.jpg
    495 KB · Views: 7
Back
Top Bottom