Mbunge Twaha Mpembenwe: Watumishi Wengi Serikalini Wanalipwa Mishahara Midogo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Twaha Mpembenwe amesema kuwa Uchambuzi wa Kamati ya Bunge ya Bajeti umebaini kwamba watumishi wengi wa Serikali wanalipwa mishahara midogo isiyoendana na kupanda kwa gharama za maisha.

Kamati imeeleza hayo wakati ikiwasilisha bungeni jijini Dodoma maoni na mapendekezo yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha pamoja na mafungu yaliyo chini yake kwa mwaka wa fedha 2023/24 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Kamati imeeleza kuwa Serikali kwa kutambua suala hili imekuwa ikiwalipa watumishi posho ili kupunguza ugumu wa maisha, jambo hili humsaidia mtumishi kwa muda anaokuwa kazini lakini halimsaidii baada ya kustaafu kwa sababu posho hazitumiki katika kukokotoa pensheni, na kwamba posho hizo zinaweza kuondolewa wakati wowote na kwamba sio chanzo cha uhakika.

Kamati imeishauri Serikali kuongeza viwango vya mishahara kwa watumishi ili kuongeza kiwango cha pensheni watakachopokea pindi wanapostaafu.

Aidha, Kamati imeshauri Serikali iangalie uwezekano wa kujumuisha kiwango cha posho katika mishahara ya watumishi ili kuongeza kiasi cha pensheni pindi watumishi hao watakapostaafu.

Screenshot 2024-06-05 at 00-12-37 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
 
Nonsense
 
Posho hizo ni kiasi gani?
Mbona haziainishwi kama wanavyoainisha makato?
Kwanini makato yafanywe kwenye gross income?
 
Back
Top Bottom