Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo aomba Rais Samia kusaidia upatikanaji tshs milioni 200 zilizotapeliwa na waliokuwa Viongozi bodoboda

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo aomba Rais Samia kusaidia upatikanaji tshs milioni 200 zilizotapeliwa na waliokuwa Viongozi bodoboda

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Jisomeeni wenyewe hapo chini kwa kiswahili:

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mrisho Mashaka Gambo amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kusaidia kufanikisha upatikanaji wa Shilingi milioni 200 zilizotapeliwa na waliokuwa Viongozi wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha, miaka minne iliyopita.

Wakati wa Mkutano mkuu wa Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha uliofanyika Ijumaa Disemba 27, 2024, mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Mohammed Kawaida, Gambo amedai kuwa watu hao wanafahamika, akiahidi kutoa milioni moja kwa kila atakayefanikisha kutiwa mbaroni kwa wahusika wa wizi na utapeli huo wa fedha za wavuja jasho.
 
Tiss ina watu wa ajabu sana..mtu km huyu, face value judgment inakupa jibu hana sifa zozote za kuwa kiongozi, mtu alikuwa mkuu wa mkoa lkn hajui jinai zinashughuliwaje..na watu wa arusha siku hizi wamekuwa mazezeta tu km wa mikoa mingine, mtu mwepesi kichwani km huyu mnaanzia wapi kumsikiliza??
 
Back
Top Bottom