Pre GE2025 Mbunge wa CCM Moshi Mjini, Priscus Tarimo aishtaki Bendi ya Polisi kwa tuhuma ya kufanya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chawa wa taifa

New Member
Joined
Nov 12, 2024
Posts
2
Reaction score
5
MAPYA YAIBUKA MOSHI, NI BAADA YA MBUNGE KUSHITAKI BENDI YA POLISI

Katika hali isiyo ya kawaida, Priscuss Tarimo ambaye ni Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini amewashtaki watumbuizaji wa bendi ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP) ambayo ilikuwa inatumbuiza kwenye sherehe ya Kumuaga binti wa Tajiri wa Moshi ndugu Didas ambaye ni Mmiliki wa Kilimanjaro Supermarket iliyofanyika tarehe 8/11/2024 katika ukumbi wa Panoni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, askari hao wamesema wametakiwa kuandika barua za maelezo kujieleza kwa nini wamefanya siasa kwenye sherehe. Wameeleza kuwa wakati wakitoa burudani ni kawaida yao kuita majina mbalimbali ya viongozi na watu maarufu ili waweze kupanda kuwatuza.

Wanasema katika sherehe hiyo alikuwepo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao waliitwa na kuitunza bendi hiyo inayofanya vizuri ndani na nje ya Mkoa. Aliendelea kueleza kuwa Mbunge wa Moshi Mjini naye aliitajwa mara kadhaa lakini hakuonesha ushirikiano.

Aidha waliendelea kuwataja watu mbalimbali wafanyabiashara na watu mashuhuri ambapo miongoni mwao alitajwa Alhaj Ibrahim Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Kapuni za Ibraline aliyefika na kuwatunza vizuri na kwa upendo mkubwa kwa kuthamini kile bendi hii ilichokuwa inakifanya.

Katika hali ya kusikitisha kitendo cha Mkurugenzi wa kampuni za Ibraline kutajwa miongoni mwa wageni waliofika kwenye hafla hiyo, kilimkasirisha sana Mbunge ambaye alichukua hatua ya Kwenda kuwashtaki bendi nzima kwa viongozi wao ambapo wametakiwa kujieleza kwa maandishi juu ya tuhuma hizo.

Kitendo hicho ni kitendo kibaya na cha kikatili ambacho kimelenga kuharibu kazi na Maisha ya wanabendi ambao ni askari wa jeshi la polisi "alisema mmoja wa viongozi wa jeshi hilo. Ingawa mbunge huyu amekuwa na tabia ya kuwashughulikia watu wote anao hisi wako karibu na Aliyekuwa mshindani wake wa nafasi ya Ubunge 2020 bila kujali athari za matendo yake kwa jamii na siasa za Moshi ambazo zimejaa upinzani.

Baadhi ya watu mbalimbali wamehojiwa juu ya malalamiko haya ya mbunge ni pamoja na Mzazi wa Bibi harusi naye amehojiwa na kueleza hali halisi ya tukio hili. Alipotafutwa Mbunge kujibu tuhuma hizi hakupokea simu yake japo ni utaratibu wake wa kutokupokea namba za waandishi wa Habari.

Mbunge wa Moshi amekuwa ni tatizo sana kwa kulinda nafasi yake. Amekuwa akilipa vijana kutukana viongozi wa chama chake akiwemo mwenyekiti wake wa wilaya sambamba na kuchapisha vipeperushi na kuvisambaza vyenye maneno ya kumchafua aliyekuwa mshindani wake.

NIlipozungumza na askari waishio ndani ya chuo cha polisi, wamesema Mbunge huyu amepoteza mvuto na ni mara kadhaa amekuwa akitumia madaraka vibaya kwa kuwachongea askari ambao hukataa kumsaidia kutoa dhamana kwa vijana wake wanapokuwa wamekamatwa kwa makosa mbalimbali.

Ikiwa jambo hili limefanyika kwa makusudi kuwaumiza polisi Chama chake hakioni kinatengeneza ajali kipindi hiki cha uchaguzi?

Kazi kwenu wanajamvi
 
Majimbo ya Moshi Mjini na Arusha mjini yanaweza kurudi upinzani kwa huu ungese unaoendelea ndani ya CCM. Ndani ya CCM kwenye hayo majimbo kuna msuguano wa hatari hali inayowapa upinzani nafasi ya kutamba. Kwa Arusha kuna mamluki kibao ndani ya CCM toka CHADEMA
 
Hata bila misuguano huko ccm, bila JPM majimbo hayo KAMWE yasingeenda ccm!.
 
Na Samia atafanya kile kile alichofanya dikteta Magufuli mfano tumeuona kwenye huu uchafuzi unaoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
MAPYA YAIBUKA MOSHI, NI BAADA YA MBUNGE KUSHITAKI BENDI YA POLISI

Katika hali isiyo ya kawaida, Priscuss Tarimo ambaye ni Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini amewashtaki watumbuizaji wa bendi ya Chuo cha Polisi Moshi (CCP) ambayo ilikuwa inatumbuiza kwenye sherehe ya Kumuaga binti wa Tajiri wa Moshi ndugu Didas ambaye ni Mmiliki wa Kilimanjaro Supermarket iliyofanyika tarehe 8/11/2024 katika ukumbi wa Panoni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, askari hao wamesema wametakiwa kuandika barua za maelezo kujieleza kwa nini wamefanya siasa kwenye sherehe. Wameeleza kuwa wakati wakitoa burudani ni kawaida yao kuita majina mbalimbali ya viongozi na watu maarufu ili waweze kupanda kuwatuza.

Wanasema katika sherehe hiyo alikuwepo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao waliitwa na kuitunza bendi hiyo inayofanya vizuri ndani na nje ya Mkoa. Aliendelea kueleza kuwa Mbunge wa Moshi Mjini naye aliitajwa mara kadhaa lakini hakuonesha ushirikiano.

Aidha waliendelea kuwataja watu mbalimbali wafanyabiashara na watu mashuhuri ambapo miongoni mwao alitajwa Alhaj Ibrahim Shayo ambaye ni Mkurugenzi wa Kapuni za Ibraline aliyefika na kuwatunza vizuri na kwa upendo mkubwa kwa kuthamini kile bendi hii ilichokuwa inakifanya.

Katika hali ya kusikitisha kitendo cha Mkurugenzi wa kampuni za Ibraline kutajwa miongoni mwa wageni waliofika kwenye hafla hiyo, kilimkasirisha sana Mbunge ambaye alichukua hatua ya Kwenda kuwashtaki bendi nzima kwa viongozi wao ambapo wametakiwa kujieleza kwa maandishi juu ya tuhuma hizo.

Kitendo hicho ni kitendo kibaya na cha kikatili ambacho kimelenga kuharibu kazi na Maisha ya wanabendi ambao ni askari wa jeshi la polisi "alisema mmoja wa viongozi wa jeshi hilo. Ingawa mbunge huyu amekuwa na tabia ya kuwashughulikia watu wote anao hisi wako karibu na Aliyekuwa mshindani wake wa nafasi ya Ubunge 2020 bila kujali athari za matendo yake kwa jamii na siasa za Moshi ambazo zimejaa upinzani.

Baadhi ya watu mbalimbali wamehojiwa juu ya malalamiko haya ya mbunge ni pamoja na Mzazi wa Bibi harusi naye amehojiwa na kueleza hali halisi ya tukio hili. Alipotafutwa Mbunge kujibu tuhuma hizi hakupokea simu yake japo ni utaratibu wake wa kutokupokea namba za waandishi wa Habari.

Mbunge wa Moshi amekuwa ni tatizo sana kwa kulinda nafasi yake. Amekuwa akilipa vijana kutukana viongozi wa chama chake akiwemo mwenyekiti wake wa wilaya sambamba na kuchapisha vipeperushi na kuvisambaza vyenye maneno ya kumchafua aliyekuwa mshindani wake.

NIlipozungumza na askari waishio ndani ya chuo cha polisi, wamesema Mbunge huyu amepoteza mvuto na ni mara kadhaa amekuwa akitumia madaraka vibaya kwa kuwachongea askari ambao hukataa kumsaidia kutoa dhamana kwa vijana wake wanapokuwa wamekamatwa kwa makosa mbalimbali.

Ikiwa jambo hili limefanyika kwa makusudi kuwaumiza polisi Chama chake hakioni kinatengeneza ajali kipindi hiki cha uchaguzi?

Kazi kwenu wanajamvi
Mnageuka wapiga wapiga debe kila kukicha kuchafua kisichochafuka
PRISCUS TARIMO BINGWAA MAMBO UNAYO FANYA TUNA YAONA TULIA KWENYE KITI CHAKO CHA UBUNGE MITANO TENA ✅
 
Back
Top Bottom