Mbunge wa Chadema Kaishia Darasa la Saba-CV Hii hapa


Tatizo pale mnapofukua za wana ccm na kuanza kuponda mnaona sawa... Lakini wa chadema si sawa
 
Misleading info. Hajaishia STD 7, ni mwalimu wa UPE.
Enzi za mwalimu alikuwa kinara huyu.
 
Sawa, kwani umeambiwa ni fisadi? Peleka ***** wako huko!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

kuwahonga wanawake zenu wewe na nani kwani ulitaka wanawake wasihongwe uhongwe wewe?basi atakuja kukuhonga wewe ili hao wanawake unaowatetea wasihongwe.
 
Da! JF kiboko naangalia topic ya Lusinde na hii naanza kuwashangaa wachangiaji kila mtu anavutia kwake, mwenye elimu ndogo akiwa kwake anamkubali kwa mwenzie hataki kabisa na inakuwa kashfa kubwa! Acheni Ushabiki
 
Adui wa ccn sio chadema, ni ukenge wa viongozi wa ccm.
Imagine Mwigulu ndo mwenye akili sana ccm... Unatefemea nini hapo!
 
Yule mbunge wa magamba mganga wa kienyeji (mchawi) mnayemuita Prof amesoma hadi wapi vile!?
Unataka tukuorodheshee uasherati ambao Rais dhaifu ameshaufanya tangu aingie madarakani? Aibu tupu.
 
Mbona hata sasa wenye CV ndogo ya hiyo wamepewa madaraka makubwa? Na bado wengine wanategemewa kupewa! Hiyo CV kubwa sana, acheni mambo ya kuangalia CV bali angalieni ujenzi wa hoja za msingi na jinsi mtu alivyojitoa kwa dhati kulitumikia taifa.
​naogopa burn
 
Labda wengine walosoma kama Opulukwa, zito , Mdee,slaa,nassari na wengineo lakin kwa Mbowe, Kasulumbai, Vicent, na wenzao wenye kaliba hiyo ushauri ni kurudi darasani haraka hapo OUT hakuna tatizo watasoma huku wakiw wanaendelea na harakati zao za kisiasa. kutetea mbumbumbu watuongoze ati kwa vile tu ni wachama chetu ni uendawazimu usiotofautiana na ule wa kova
 
KWANI MURUTUNGURU T. COLLEGE NI PRIMARY SCHOOL??
DAH WANACHUKI BINAFSI yoyoyo Eh Eh.... ALI CHOKI Et al.
 
Misleading info. Hajaishia STD 7, ni mwalimu wa UPE.
Enzi za mwalimu alikuwa kinara huyu.

wajua tuna wadharau walimu wa upe, hawa ndo walikuwaCream katika madarasa yao enzi izo, Dr. Bana, Profesa Mallya mkono hawa wote walitoka kama walimu wa upe, wakajiedeleza mpake leo hivi ni maprofesa,
 
huyu jamaa alikuwa cuf! Ndo akaja chadema! Honestly hana elimu alafu ni dhulma mno!
 
Hii CV ina walakini.Mbona hata miaka ya Shule ya Msingi haionekani hapo? Umejuaje kama amemaliza darasa la saba? Chochote kilichopo kwenye mtandao wa Bunge kina walakini.Usikiamini sana...utashusha heshima yako bure.
 
Haya Mkuu, Nchi hii imeshafikia kuongozwa na ma Dr , na kwa kulitambua hilo leo tuna Dr JK na tutaendele kushuhudia ma Dr wajao usishangae ukasikia Dr EK 2015 , yetu maho tutasikia mengi
 
Tungeangalia idadi ya Watanzania watu wazima ni wangapi (zaidi ya miaka 20) tufanye ni 45% ya idadi ya watanzania milioni 40 -- Idadi ya Watanzania watu wazima ni takribani 18,000,000; swali kati ya hawa Watanzania watu wazima 18,000,000 ni wangapi wenye hiyo elimu ya shahada ya chuo kikuu?

Na swali la pili wale wasiokuwa na elimu ya chuo kikuu hawahitaji kuwakilishwa?

Swali la tatu kwa kila jimbo lililo na Mbunge, unafikiri Mbunge msomi mwenye PHD ambaye makazi na familia yake yako DSM anaweza kweli kuchangamana na tabaka la walala hoi, kuchukua mawazo yao na kwenda kuwasemea Bungeni?
 
Jamani hivi Mwalimu wa Primary naye mnamchukulia darasa la 7 wakuu
 
Ruksa. Awe mtanzania halisi na ajue kusoma na kuandika. Hakuna sheria ilovunjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…