Mbunge wa chadema kortini

mwanaone

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
637
Reaction score
760
Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Meatu, Meshack Oporukwa (Chadema), baada ya kushikiliwa kwa saa 24.

Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu kutoa mkoani humo, Oporukwa alisema aliachiwa kwa dhamana jana saa 8:30 alasiri baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Oporukwa alisema alisomewa mashitaka mawili ambayo ni ya kuitisha mkusanyiko usio halali na shitaka la pili ni kukaidi amri ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa kuitisha mkutano usio halali.

Oporukwa alisema mahakama ilimtaka awe na wadhamini wawili na mali zisizohamishika zenye thamanai ya Sh. 500,000 kila mmoja.

Alisema alidhaminiwa na mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rachel Mashishanga na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Shinyanga, Yasine Swedi.

Kesi hiyo ilihairishwa hadi June 2, mwaka huu.

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga lilimkamata mbunge huyo baada ya kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nkoma, wilayani Meatu alipokuwa anawashukuru wananchi kwa kumpigia kura na Jeshi la Polisi lilidai kuwa alivunja sheria kwa kufanya mkutano wa hadhara na kuzidisha muda.

CHANZO: NIPASHE
 
Cdm fuateni maagizo toka kwa mamlaka husika vinginevyo muda mwingi mtatumia katika viwanja vya mahakama
 
Mambo mengine ni ya kuyamaliza kwa busara tu!...Polisi wanataka waonekane wako kazini!
 
mimi naona bora tuandamane ili kesi ifutwe kwani huu ni uonevu.
 
Hamna cha ajabu, hata mandela alisimama mahakamani. Vita mbele kwa mbele, hatubabaiki. Cha moto mtakiona safari hii. CCM wakiitisha mikutano hawaombi vibali, wanafki wakubwa.:israel:
 
Huu ni uonevu mkubwa na siku si nyingi uvumilivu utakwisha na nchi yetu itakuwa kama Egypt. Sioni sababu ya kumzuia mbunge asifanye kazi zake ambazo ni pamoja na kuwasikiliza watu waliomchagua. Hawa polisi manduli iko siku itawatokea puani.
 
dawa tuitishe maandamano nchi nzima ili kesi zote za viongozi wa chadema na wafuasi zifutwe. na wafungwa wote wa ambao watakuwa wanaiunga mkono chadema waachiwe kutokana itakuwa wanaonewa.
 
HUMAN RIGHT ACT
Article 11: Freedom of Assembly
(1) Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and to freedom of association with others, including the right to form and to join trade unions for the protection of his interests.
(2) No restrictions shall be placed on the exercise of these rights other than such as are prescribed by law and are necessary in a democratic society in the interests of national security or public safety, for the prevention of disorder or crime, for the protection of health or morals or for the protection of the rights and freedoms of others.
This Article shall not prevent the imposition of lawful restrictions on the exercise of these rights by members of the armed forces, of the police or of the administration of the state.

HAO WANANCHI HAKUNA ALIYEKWENDA KULALAMIKA POLISI KWA TUKIO HILO
ILA WAO POLISI KWA KUTUMWA NA CHAMA KWA MASLAHI YA CHAMA WANAONA HUYO MBUNGE NI TATIZO KAMA ATAJICHANGA NA WANANCHI
kwa wale wasiojua ni kwamba mbunge alikuwa na wananchi wake kwenye mechi ya mpira (mchangani) yeye alikuwa mgeni rasmi polisi wakasema amevunja sheria kwa kufanya mkutano nje ya masaa yanayoruhusi,
na hapo ilikuwa mpirani na hakuna mkutano wala siasa
mimi nachoona ni kwamba wanaona jamaa anajijenga kisiasa hapo jimbo vizuri, maana wabunge wa vyama vyao uchaguzi ukipita ndio uwaoni tena,


Cdm fuateni maagizo toka kwa mamlaka husika vinginevyo muda mwingi mtatumia katika viwanja vya mahakama
 
Mhmm Polisi wa Nchni Maskini hata akili inakuwa Maskini Kiasi hicho?

Hiyo ndio Polisi ya Tanzani asilimia 90 ni vyeti vya kufoji vya form four, unategemea nini Hakuna Polisi huko mikoani hata mmoja aliyefika level ya degree! na wengi wao ni wale walioingia katika hilo jeshi kwa vyeti vya ndugu na majina bandia.
 
Huu ni uonevu mkubwa na siku si nyingi uvumilivu utakwisha na nchi yetu itakuwa kama Egypt. Sioni sababu ya kumzuia mbunge asifanye kazi zake ambazo ni pamoja na kuwasikiliza watu waliomchagua. Hawa polisi manduli iko siku itawatokea puani.
kama ndoto yako tanzania iwe kama misri kaka au ww dada umechelewa na utasubiri mpaka yesu atarudi
K
 
kaka ungetoa tu maelezo ya nn kilitokea ila hizo citation za sheria zina maana pana zaid na cdhan hata kama umeziielewa vizuri..maana zinaenda tofaut na matakwa yako..karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…