Mbunge wa Chwaka azungumzia miundombinu ya elimu - wilaya ya kati, mkoa kusini Unguja

Mbunge wa Chwaka azungumzia miundombinu ya elimu - wilaya ya kati, mkoa kusini Unguja

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MBUNGE WA CHWAKA AZUNGUMZIA MIUNDOMBINU YA ELIMU - WILAYA YA KATI, MKOA KUSINI UNGUJA

Mbunge wa Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Haji Mlenge katika kuonyesha utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 kupitia miundombinu ya Elimu katika jimbo la Chwaka ameonyesha miundombinu mbalimbali iliyoboreshwa na kuzidi kutengeneza mazingira rafiki kwa Wanafunzi kusoma na kutimiza ndoto za maisha yao.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akitembelea Shule Mpya na Shule zilizofanyiwa ukarabati, Shule za Awali na Shule za Sekondari kwa masomo ya sayansi Mhe. Haji Mlenge ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto ya madarasa.

Aidha, Mhe. Haji Mlenge ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchukua hatua dhabiti za kuhakikisha wanafunzi wote wanapata mazingira rafiki ya kujifunzia.

Mwisho, Mhe. Haji Mlenge wakati akiendelea na ziara yake amewasisitiza wanafunzi kuwa na juhudi katika masomo kwani itawawea rahisi kutimiza ndoto za Maisha yao.

#UchumiWaBuluu
#KaziIendelee
 

Attachments

  • IMG-20230125-WA0079.jpg
    IMG-20230125-WA0079.jpg
    114.4 KB · Views: 2
  • IMG-20230125-WA0085.jpg
    IMG-20230125-WA0085.jpg
    104.9 KB · Views: 2
  • IMG-20230125-WA0083.jpg
    IMG-20230125-WA0083.jpg
    111.8 KB · Views: 2
  • IMG-20230125-WA0082.jpg
    IMG-20230125-WA0082.jpg
    100.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom