Mbunge wa Jimbo la Hai anza kufungasha mizigo yako mapema

Mbunge wa Jimbo la Hai anza kufungasha mizigo yako mapema

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kwa masikitiko makubwa, kila Jimbo Tanzania linapokea fedha za mfuko wa Jimbo kwa maendeleo ya Jimbo. Huu ni mwaka wa 3 Jimbo la Hai halijawahi kuona au kupokea fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo ya Hai.

Mbunge Saashisha Mafue akiulizwa anataka kukata watu na mapanga. Mfuko huo hauna kamati wala haijulikani kama Mbunge anapewa fedha za mfuko wa Jimbo.

Kwa Hali ilivyo fedha zote zitalipwa na mbunge Saashisha na tunamtangazia kuwa aanze kufungasha virago mapema ampishe kijana mwenzake ambaye ameanza kuanzisha hata timu za mipira na kuchangia maendeleo ya Jimbo la Hai.

Saashisha anza kufungasha mizigo mapema.
 
Wabunge wa Magufuli hapo, wana chukua chao mapema anajua uchaguzi ujao hana nafasi ya kurudi hapo.

Majimbo yote Tanzania yanapokea pesa za mfuko wa jimbo asikudanganye mtu, mumuulize hizo pesa anapeleka wapi?
 
Back
Top Bottom