Miongoni mwa Wabunge wa Tanzania waliobahatika kuteuliwa kufanya ziara ya siri huko Dubai, yumo mbunge wa Jimbo la Msalala la Mkoani Shinyanga.
Taarifa zinaonesha kwamba Mbunge huyu alivyorudi tu yeye hakutaka kununua gari la kuandika jina lake kama alivyofanya Musukuma, bali yeye ameamua kugawa nyama ya ng'ombe kila kijiji, ambako kijiji kimoja kimeambulia ng'ombe kubwa mbili.
Ikumbukwe kwamba Jimbo la Msalala lina kata 18, ambapo kila kata ina vijiji 6, unadhani wabunge walioenda kule walilipwa bei gani kila mmoja na kwanini walipwe vitita vyote hivyo?
Toa Maoni yako.

- Tunachokijua
- JamiiForums imefuatulia suala hili na kubaini kuwa ni kweli ng'ombe waligawiwa lakini hawajatolewa na Mbunge. Chanzo chetu kimedai kuwa Mradi huo wa ng'ombe ni wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye anadaiwa katoa Ng'ombe 50 wa kisasa kwa Wanavikundi wa vijiji mbalimbali.
Huu ni mradi wa mikoa mbalimbali sio Jimbo la Msalala pekee ambapo Ng'ombe akizaa hupatiwa mwananchi Mwingine. Na Kila Mwanakijiji ana haki sawa ya kumiliki ng'ombe hao.
Suala hili halihusiani na yanayoendelea kati ya Serikali na Kampuni ya DP WORLD ya Dubai.
Zaidi ya chanzo hicho, JamiiForums pia imepitia orodha ya Wabunge walioenda Dubai na kubaini kuwa mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi sio sehemu ya wabunge 30 waliopafa nafasi ya kutembelea Dubai ili kujiridhisha juu ya ufanisi na utendaji kazi wa kampuni ya DP World.
Orodha hiyo ilichapishwa JamiiForums Juni 17, 2023 kwenye andiko lililo na kichwa cha habari “Orodha ya wabunge walioenda Dubai”.
Orodha ya wabunge waliokwenda DubaiHivyo, orodha hiyo ni uthibitisho mwingine unaoleta mashaka juu ya hoja iliyotolewa na mdau ambayo pamoja na mambo mengine alidai kuwa Mbunge Iddi Kassim Iddi alikuwa miongoni mwa wabunge 30 waliotembelea Dubai kwa siri.