Mbunge wa Kabete Nairobi, Mh. George Muchai auawa kwa kupigwa risasi

commonmwananchi

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,377
Reaction score
1,956
Kwa mujibu wa televisheni ya ntv ya Kenya.

Mheshimiwa ameuawa pamoja na dereva wake pamoja na walinzi wake wawili majira ya saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo katkka barabara ya Kenyatta avenue wakati akiwa njiani kutoka katika sherehe.

Alisimama na ili kununua magazeti,na ndipo mtu aliyevalia mask alipojitokeza kutoka gari ndogo aina ya toyota pro-box na kuanza kuwafyatulia risasi vichwani kila mmoja,akitumia bunduki aina ya AK 47.

Pia alipora briefcase ya marehemu pamoja na bastola mbili za walinzi wake na kutokomea kusikojulikana akitumia gari hilo lililokuwa limefichwa namba zake.

Marehemu pia alikuwa ameambatana na mke na watoto wake wawili wa kike waliokuwa ndani ya gari la nyuma na walishuhudia mauaji hayo yakifanyika.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Kenyatta hospital Nairobi.

R.I.P marehemu wote.

 

Attachments

  • 1423289426568.jpg
    38 KB · Views: 2,050
Pole sana Mh Mbunge
Mungu Ailaze Pema Peponi Roho ya Mh
 
Pana jambo. Si hvhv.

Ni kweli maana eneo lile la nyayo lilikuwa na askari kadhaa karibu na eneo la tukio na hawaluonekana kufanya lolote.
Hii ni kwa mujibu wa muuza magazeti shuhuda wa tukio.
Pia huyu anakuwa mbunge wa pili kutoka kiambuu kuuliwa mkuu
 
poleni wafiwa...poor victims caught off guarded....
 
Very Sad indeed! ... May they RIP
Kabete MP George Muchai shot dead outside Nyayo House in Nairobi. His driver, bodyguard and another passenger also killed. Police say masked gunmen in a Probox trailed them from Westlands



 
Ni kweli maana eneo lile la nyayo lilikuwa na askari kadhaa karibu na eneo la tukio na hawaluonekana kufanya lolote.
Hii ni kwa mujibu wa muuza magazeti shuhuda wa tukio.
Pia huyu anakuwa mbunge wa pili kutoka kiambuu kuuliwa mkuu

Ajabu ni kwamba huyo muuaji ni kama hakuwa na wasiwasi wa kukamatwa kwani aliwapiga risasi na kuwaua wote wanne yaani mbunge, walinzi wawili na dereva.

Halafu pia akachukua bastola mbili za walinzi na briefcase ya mbunge na kuondoka zake.

R.I.P mbunge na wenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…