Pre GE2025 Mbunge wa Madaba Dkt.Joseph Kizito Mhagama, atembelea kata ya Mkongotema kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo

Pre GE2025 Mbunge wa Madaba Dkt.Joseph Kizito Mhagama, atembelea kata ya Mkongotema kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mbunge wa Jimbo la Madaba Mkoani Ruvuma, Dkt.Joseph Kizito Mhagama, ametembelea kata ya Mkongotema kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo hilo.

Ziara hiyo imewapa wananchi nafasi ya kueleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika hotuba yake, Mbunge Mhagama ameishukuru Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule, zahanati, miradi ya maji safi na salama, pamoja na usambazaji wa umeme katika vijiji mbalimbali.

Akitolea mfano wa mafanikio hayo, Mhagama amekitaja kijiji cha Lutukila kama moja ya maeneo yaliyopokea huduma hizo kwa ufanisi mkubwa. Pia, ameongeza kuwa kijiji cha Ndelenyuma hapo awali kilikuwa na changamoto kubwa, lakini kwa sasa huduma muhimu kama maji, elimu, umeme, ujenzi wa ofisi za kijiji, na miundombinu ya barabara zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa bajeti kiasi cha shilingi bilion na milioni moja na ishirini .

Mwenyekiti wa kijiji cha Ndelenyuma Stanley Ngailo amepongeza juhudi za Mbunge Mhagama kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kijiji chao.
1740241509460.jpg
1740241505538.jpg
 
Back
Top Bottom