Mbunge wa Jimbo wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi amemaliza changamoto ya Umeme, Maji na Choo katika Soko la Chita jimboni humo baada ya kutoa Sh Milioni 1.5.
Mbunge wetu wa Mpwapwa unaona wabunge wenzako wanavyosonga mbele serikali itawafuata nyuma wewe umebaki kuitisha misa tu badala ya kupambana.
Changamoto za jimbo la Mpwapwa zinajulikana mtu anaweza hata kuziimba kama ndege, unangoja nini? Utazitatua huko kanisani unakoshinda unasali?
Labda nikusaidie:
1. Barabara ya lami toka mbuyuni Kongwa hadi Mwanakiyanga Mpwapwa- Hii ni changamoto kubwa hata miaka miwili ikiwa bado tutakuelewa lakini inabidi uanze mahali.
2. Maji, maji ya baridi huu eti ni mradi wa watu kujipatia kipato . si unaona mikokoteni na baiskeli na madumu barabarani? Hii ya uuzaji maji inabidi uiondoe. kwani maji yako chini kidogo tu tukichimba tutayakuta, mradi wa kuuza maji inabidi uumalize
3. Jokofu la mochwale hospitali ya wilaya siyo zuri sana maiti zinaharibika haraka liangalie.
4. Bima za afya walioisha kata fuatilia wapate huduma
5. Buni vyanzo vipya vya mapato, makusanyo ya mapato ya halmashauri ni hafifu, ni vigumu kufikisha malengo kwa vyanzo vilivyopo inabidi ulivalie njuga pamoja na madiwani ukizubaa ulete siasa unajua kitakachotokea serikali awamu hii haina mchezo mchezo
6. Elimu. Elimu shule za secondali ziboreshwe hizi hizi zilizopo, Maabara za masomo ya sayansi ziboreshwe na anzisha vyumba vya kompyuta. TEHEMA kipindi hiki ndo habari ya mjini, boresha zilizopo siyo lazima kuanzisha zingine, toka kanisani tembelea mashuleni, shule za msingi na secondari zungumza na walimu upate vilio vyo uvifikishe serikalini kupitia vikao vya bunge.
7. Vifo vya akina mama wajawazito,fuatilia watumishi afya kwenye zahanati n VITUO VYA AFYA. sikiliza vilio vyao ili uwapandishe morale wa kazi pia ukaangalie akina mama ngojea pale hospitali ya wilaya ujilizishe na mazingila wanayoishi.
8. Anza mchakato inatakiwa vijiji vya Bumila, Chibwechangula na Lupeta wapate zahanati na iwe Chibwechangula ili iwe rahisi kuhudumia vijiji hivyo vyote masuala ya chanjo kwa watoto na akina mama wajawazito pia na masuala mengine ya afya, hili yule uliyemrithi alinasibiwa kwamba aliuliza masuali mengi kuliko mbunge yoyote , maswali 103 hilo la zahati eti hakuuliza, sijui sasa alikuwa anauliza nini.
9. VETA , kuwepo kwa mafunzo ya VETA kunahitajika sana Mpwapwa kuliko hata Chato, VETA Mpwapwa inalipa sana ikiwepo, hiyo ni changamoto anza nayo ili Mpwapwa iwe kama sehemu zingine
10. Umeme. umeme Mpwapwa umekuwa wa kubahatisha hasa kipindi hiki chako mbunge. Umeme ni maisha unakatika kila siku saa ingine masaa 24, fuatilia kuna nini? Umeme mheshimiwa mbunge usipofuatilia ujue tatizo ni nini unatosha kabisa kukung`oa.
Toka huko kanisani unakosali, ingia mtaani, angalia wenzio wanavyochachalika. Mlungu ntaza hanze nolumanko.
Rais anapeleka maendeleo Chato, na wewe Mbunge yalete jimbo la Mpwapwa
Aksante Mh .Mbunge nakutakia kazi njema sikulaumu chochote bado ndio umeanza ila nakusaidia tu uanzeje.