Mbunge wa Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchafuliwa baada ya kugundua kuwepo kwa miradi hewa na matumizi mabaya ya fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC). Mbunge huyo anaungana na Madiwani wengi wanaotaka Tume ya Uchunguzi iundwe. Mkurugenzi aliyehama na Mwenyekiti wa Halmashauri hawataki Tume hiyo iundwe. Inadaiwa hiki ndicho chanzo cha kumchafua Mbunge huyo.