Mbunge wa Ngorongoro ang’ang’ania Loliondo wanaonewa

Mbunge wa Ngorongoro ang’ang’ania Loliondo wanaonewa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa wakazi wa Loliondo wanaonewa, kuumizwa na kudhulumiwa haki zao wakati ardhi ni haki yao.

Ole Shangai amerudia tena msimamo wake kuwa kuna wananchi wake ambao waliumizwa na lakini wakanyimwa PF3 na hivyo kuwafanya wakatibiwe nchini Kenya.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Juni 22,2022 bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu ya Serikali akisema kuna upotoshwaji mkubwa kwenye sakata la Loliondo.

Licha ya kupewa taarifa na wabunge wenzake wakati akichangia bajeti hiyo, Shangai amesema kinachofanyika Loliondo ni uonevu kwa wapiga kura wake.

Amesema wabunge wengi wanaozungumzia suala la Loliondo ni kwa sababu hawajui lakini yeye anajua kwa sababu wanaoguswa ni wapiga kura wake.

Tangu kuanza kwa mgogoro wa Loliondo ambapo Serikali imeweka alama za mipaka na kuchukua eneo la kilometa 1,500 za mraba kwa ajili ya uhifadhi, mbunge huyo amekuwa akitoka mbele ya vyombo vya habari na kuzungumzia anachokiita ni mateso ya wananchi wake katika ardhi yao.

“Najua kuna watu wanacheka humu, lakini mimi nazungumzia maisha ya watu wangu, babu zangu, baba zangu, kaka zangu na wadogo zangu ile ni ardhi yao,” amesema Ole Shangai.

Mbunge huyo licha ya kutakiwa na Mwenyekiti wa bunge Najma Giga afute kauli yake kuhusu wananchi kutibiwa Kenya kama hana ushahidi, lakini hakufanya hivyo kwa kile alichosema ana ukweli na anachokizungumza

Shangai ameitaka Serikali kufikiria upya namna inavyoweza kupitia upya mipaka ya eneo hilo ili kuwapa haki wananchi ambao amesema hawajashirikishwa kwa jambo lolote.
 
Mwambie atafute pa kuhamishia mifugo yake, janja janja hakuna tena
 
Hivi si mjadaia wa loliondo ulifungwa jana
 
Back
Top Bottom