Habari wadau.Napenda kumpa taarifa mbunge wa NYAMAGANA bwana mabula kuwa ukiondoa matatizo mengi yaliyopo wilaya ya hii ambayo ni kitovu cha uchumi wa mkoa kama ukosefu wa huduma ya maji na barabara mbovu kuna aibu ambayo naomba yeye binafsi aifuatilie.Hii aibuu ya watoto kwenda na magunia kwenye mabegi ya madaftari kwa ajili ya kwenda kukalia darasani inatia uchungu saana.Yaani unakuta darasa lina madawati 2 watoto 200.Watoto wanatandika magunia darasani ni kama wapo vitani!
Na kwa serikali umefika wakati sasa wakiri kuwa utoaji wa elimu bure umeshindikana hivyo warudishe ada ili tuache kutesa watoto.
Naomba kumtajia jina la shule hiyo na wadau wengine ambao mpo jijini MWANZA mnaweza kufika kujionea maajabu ya Karne ili tuone tunawasaidia vipi??
Shule ya msingi Nyangulugulu kata ya Mahina.