Mbunge wa Ruangwa Lindi afariki dunia

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
4,692
Reaction score
3,891
leo tena majira ya saa sita na robo usiku mbunge wa RUANGWA mkoani LINDI MHE. SIGFRIDI N'GITU ameaga dunia katika hospitali ya moi kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu, mungu amlaze marehemu mahali pema peponi amina.

bunge limeharisha kikao chake leo asubuhi kwa mujibu wa kanuni
 
Bwana mkubwa wa shamba anaendelea kufanya kazi yake ya kuvuna, kazi yake na haina makosa!

RIP........!

PHD ...ingefaa uiweke hii kule kny matangazo madogo madogo
 

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana liidimiwe. Mzee hapo mbona umetumia 'thumb up' kulikoni?
 
salaam nyingi kwa Amina Chifupa na Chacha Wangwe, waambie huku bunge linaendelea , na jumaatano kuna Historia mpya itaandikwa nchi hii.
PUMZIKA KWA AMANI.
 
salaam nyingi kwa amina chifupa na chacha wangwe, waambie huku bunge linaendelea , na jumaatano kuna historia mpya itaandikwa nchi hii.
Pumzika kwa amani.
r.i.p
 
N'gitu huyu anauhusiano na yule mfanyabiashara wa mabasi,au ndio yeye mwenyewe?But any ways Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu!!!
 
Poleni sana Wafiwa, Spika na wapiga kura wake. 2010 wagombea wapimwe vizuri afya zao.
 
Nawapa pole wafiwa wote waliokutwa na msiba huu,Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.
 
Poleni wafiwa, poleni wananchi wa ruangwa, Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, amin.
 
salaam nyingi kwa Amina Chifupa na Chacha Wangwe, waambie huku bunge linaendelea , na jumaatano kuna Historia mpya itaandikwa nchi hii.
PUMZIKA KWA AMANI.

Historia gani tena Nguvumali? Hebu nipe Data m2 wangu
 
Unajuaje kwamba watakutana? inawezekana mmoja alipita njia nyembamba na wengine njia pana, hapo hakuna kukutana maana destinations zinakuwa tofauti.
Poleni sana wafiwa. Kuweni na uvumilivu na hali iliyowakuta. Kila mmoja wetu ataonja mauti. Jiwekeni tayari kwa jambo hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…