Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa kuanza kuendesha bodaboda kuanzia Novemba 2 ili kuwaunga mkono bodaboda wote Tanzania

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa kuanza kuendesha bodaboda kuanzia Novemba 2 ili kuwaunga mkono bodaboda wote Tanzania

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Ni yeye Silaa

Amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam

Silaa ambaye ni Mbunge wa kuchaguliwa akiwakilisha jimbo la uchaguzi la Ukonga amesema nia yake hiyo ni kutaka kuonyesha umoja na madereva wote wa bodaboda nchini Tanzania.

Ikumbukwe, Mamlaka za Serikali ndani ya mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni zimetoa tangazo la kuzuia vijana waendesha bodaboda na bajaji kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Heading ilipaswa iwe.

Jerry Silaa Mbunge wa Ukonga kuanzia kesho ataanzisha vuguvugu kwa kuendesha bodaboda ili kuwaunga mkono bodaboda wote Tanzania.
 
Huyu dogo nae kwa kutafuta makubwa hajambo!

Jerry ulikuwa na nafasi nzuri sana wakati wa JK sijui ulikosea nini ukatolewa kwenye reli, kwa umri wako tulia. Tulia kabisa utakuja kutoka baadae ila usitafute Kiki kwa mihemko. Tulia wewe bado mdogo, kuwa humble kama unaipenda siasa. Ukilazimisha makiki sasa hivi mdogo wangu utaisahau siasa mazima.

Angalia hao kina JK walianziaga siasa zao Nachingwea huko tena kwa nafasi za kawaida sana ni utii tu na kunyenyekea ndio uliwafikisha waliopofika. Kama unahitaji siasa hizo ulizomo hapo tulia ila kama unahitaji kupingana na hilo dubwana ulilo ndani yake na uje utoke kivyako vyako basi soma nyakati vizuri na ukiona ni sawa endelea na huo uanaharakati wako.
 
Again, bodaboda mnaanza kutumika na wanasiasa na nyie mnakubali.... Ndio yaleyale ya jamaa mmoja kujifanya rafiki zenu, kupanda daladala siku moja ilihali watu wanapanda kila siku, kula kwa mama ntilie akizitafuta kura za wananchi leo hii hatumuoni tena akipanda daladala wala kula chakula cha mama ntilie..
 
Tusubiri kidogo wa Ilala nae aache V8 aendeshe boxa

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimetafakari sana

Screenshot_20211101-133128.jpg
 
Likimvunja mguu je!

Hawa wanasiasa kila jambo wanalirukia tu

Badala ya kuja na utaratibu,suluhisho khs boda

Ova
 
Hiyu dogo nae kwa kutafuta makubwa hajambo!

Jerry ulikuwa na nafasi nzuri sana wakati wa JK sijui ulikosea nini ukatolewa kwenye reli, kwa umri wako tulia. Tulia kabisa utakuja kutoka baadae ila usitafute Kiki kwa mihemko. Tulia wewe bado mdogo, kuwa humble kama unaipenda siasa. Ukilazimisha makiki sasa hivi mdogo wangu utaisahau siasa mazima.

Angalia hao kina JK walianziaga siasa zao Nachingwea huko tena kwa nafasi za kawaida sana ni utii tu na kunyenyekea ndio uliwafikisha waliopofika. Kama unahitaji siasa hizo ulizomo hapo tulia ila kama unahitaji kupingana na hilo dubwana ulilo ndani yake na uje utoke kivyako vyako basi soma nyakati vizuri na ukiona ni sawa endelea na huo uanaharakati wako.
Mama samia anakazi kubwa sana kwakweli kwasasa ndio naelewa kwa nini magufuli aliendeaha hii nchi kwa mkono wa chuma kumbe kuna mambo ukiyachekea yanaliingiza taifa kwenye tatizo.
 
Wewe na wapumbavu wenzio Magufuli anahusika nini? Kila siku magufuli hata ukishinda kumlizisha mkeo Magufuli! Nchii hii sio ya CCM wala Magufuli pambaneni na hali zenu ni wakati wenu nyinyi Mafisadi!
We jamaa umakwama maisha nini maana hili ni povu la cleesoft.😁😂😂😂😂
 
Huyu ndio yule alienda na begi 2 za vitabu vya sheria ili kwenda kujitetea akihojiwa na kina Msukuma.
No wonder Musukuma anawadharau Sana wasomi walioko Bungeni..
 
Back
Top Bottom