Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE BUPE MWAKANG'ATA AKICHANGIA HOJA YA BAJETI YA WIZARA YA KILIMO
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa Mhe. Bupe Mwakang'ata tarehe 09 Mei, 2023 alichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo iliyosomwa Bungeni na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe.
"i. Mfano, sisi Mkoa wa Rukwa Mbegu tunatoa Zambia 🇿🇲 na hatujui ubora wake. Serikali ianzishe haya Mashamba ya Mbegu ili tuache kuagiza za nje ambazo hazina ubora katika maeneo yetu" - Mhe. Bupe Mwakang'ata
"Hii benki ya Kilimo kwa sasa ipo Dar es Salaam mahali ambako watu wengi sio wakulima. Kwanini isifunguliwe matawi mikoani au hata kwa baadhi ya Mikoa ili kuwasogezea wakulima huduma" - Mhe. Bupe Mwakang'ata
"Niombe pia hizi haya Mashamba ya Mfano yaanzishwe pia mikoani mingine kama Rukwa, Mbeya na hata Kigoma. Isiwe tu Dodoma. Tukianzisha haya Mashamba katika mikoa mingi tutapata vijana wengi watakaoshiriki na kujiajiri" - Mhe. Bupe Mwakang'ata
"Huu mradi wa BBT ni mzuri sana lakini Naomba uhusishe pia wanawake isiishie tu kwa vijana. Wanawake ni wazalishaji wazuri na ukiwawezesha wanawake umeiwezesha Jamii" - Mhe. Bupe Mwakang'ata
"Serikali imetoa Pikipiki 7000 kwa maafisa Ugani nchini waweze kufika kwa wakulima kutatua changamoto zao. Lakini hatuoni wakichakalika sana kwa wakulima. Kama tatizo ni mafuta niombe wapatiwe ili kazi ifanyike vizuri" - Mhe. Bupe Mwakang'ata
"Naomba hii bodi ya mazao mchanganyiko iweze kuongezewa pesa. Pamoja na kuwa inajiendesha kibiashara lakini bado haijakuwa na uwezo wa kununua mazao mengi. Naomba iongezewe mtaji ili iweze kujiendesha kwa ufasaha" - Mhe. Bupe Mwakang'ata.