Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. ENG. MWANAISHA ULENGE ASHIRIKI MKUTANO WA 146 WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI MANAMA, BAHRAIN
Mbunge wa Viti Maalum (Wanawake) Mkoa wa Tanga, Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge ni miongoni mwa wabunge wa Tanzania walioshiriki Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoongozwa na Spika wa Bunge la JMT Mhe. Dkt. Tulia Ackson nchini Bahrain.
Katika kikao cha Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Ulenge alipata nafasi ya kuchangia kuhusu mjadala wa hoja ya dharura ya kuwasilishwa na hatimaye ikubaliwe na Umoja wa Mabunge ya Dunia. Mhe. Ulenge aliunga mkono hoja ya kuanzishwa kwa mfuko wa dunia wa maafa yatokanayo na mabadiliko ya Tabia nchi (Green Climate Fund).
Mkutano huo unaofaofanyika Nchini Bahrain kuanzia Machi 9-15 unaongozwa na Rais wa Umoja wa Nchi za Afrika ambazo ni wajumbe wa Umoja wa Mabunge duniani (Africa geopolitical group) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Katika ziara hiyo, Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson ameambatana na Wabunge Wawakilishi kwenye Umoja huo ambao ni Mhe. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu, Mhe. Eng. Mwanaisha Ulenge, Mhe. Ramadhan Ramadhan, Mhe. Faustine Ndugulile pamoja na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa J. Mwihambi, ndc.