The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wakuu
Mbunge wa Viti Maalum, Sylvia Sigula, amezindua kituo cha mafunzo ya ushonaji, urembo, mapambo, na ujasiriamali kwa vijana wa Mkoa wa Rukwa, ikiwa ni hatua ya kuwawezesha kujiajiri na kupunguza changamoto ya ajira.
Kituo hicho kipo chini ya Taasisi ya Sigula Wezesha Foundation, ambayo inaendeshwa na mbunge huyo, na tayari kimesajili vijana 42 katika awamu ya kwanza. Wanafunzi hao watapata mafunzo ya miezi mitatu bila malipo, wakifundishwa na walimu wenye ujuzi na uzoefu. Baada ya kuhitimu, kila mmoja atapatiwa cherehani bure ili aweze kujiajiri.
Soma Pia: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa aliunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia shilingi 300,000 kwa ajili ya kununua vitambaa vya kujifunzia.
Naye Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aesh Hilary, alichangia shilingi 2,000,000 kwa ununuzi wa kompyuta pamoja na cherehani 10 zenye thamani ya shilingi 3,000,000 ili kuongeza uwezo wa kituo kuandikisha vijana wengi zaidi.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Sylvia Sigula, amesema lengo lake ni kuwawezesha vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi na kujikwamua kutoka kwenye changamoto za ajira.
Katika hatua hiyo, viongozi na wadau wa maendeleo wamepongeza juhudi za taasisi hiyo, wakisema ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuinua maisha ya vijana.