Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu.
Wabunge wa CCM washaanza kutoa siri za kambi
Mbunge wa viti maalum Jesca Kishoa hivi karibuni akiwa nanaongea na wananchi amefichua kuwa aliwahi kushauriwa na kiongozi mmoja wa kisiasa kwamba abadili mbinu zake za kisiasa na kwamba badala ya kuwahudumia wananchi, aweke akiba ya fedha kwa ajili ya kutoa hongo wakati wa uchaguzi.
kizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nkalakala, Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida, tarehe 16 Februari, 2025 Kishoa amesema:
"Aliniambia, ‘Jesca, tunza fedha zako, cheza na wajumbe. Unatumia njia ndefu mno. Kipyenga kikipulizwa, zitumie kuwahonga wajumbe ikiwa utagombea kupitia CCM au chama chochote.’
Katika ziara hiyo, Mhe. Jesca Kishoa alizungumza na wananchi na pia alitoa mchango wa zaidi ya shilingi milioni 6 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo. Aligawa mitungi 40 ya gesi kwa mama ntilie, seti 12 za jezi kwa timu mbalimbali, na shilingi laki tano kwa mama mwenye mtoto mwenye ulemavu.