Mbunge wa Viti Maalumu Subira Mgalu awafunda UWT Kata ya Kerege Bagamoyo

Mbunge wa Viti Maalumu Subira Mgalu awafunda UWT Kata ya Kerege Bagamoyo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
IMG-20241013-WA0370.jpg

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani Mhe. Subira Mgalu azungumza na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kerege iliyopo Bagamoyo Pwani tarehe 12 Oktoba, 2024.

Mkutano huo wenye lengo la kuzindua "Kamati za Ushindi" ulilenga katika kuhamasisha na kutoa elimu ya uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kuwa Wananchi wote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha.

Kama ilivyo jina la kata yenu KEREGE CCM tunategemea kwa jina hili mtapata ushindi kwa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi katika vitongoji vyote.

Nawasihi umoja wetu kama wanachama uonekane katika kujiandikisha na kuwepo katika siku husika ya kupiga kura.

IMG-20241013-WA0368.jpg

Nawaletea salamu za Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan yeye ameshajiandikisha jana na anawasihi nanyi mjiandikishe, maendeleo yatakuja kwa wingi katika kata hii ondoeni shaka" Subira Mgalu

"Wakati wao chadema wanashinda mitandaoni sisi tuko safi na vizuri na tupo kidigitali na wote tumejisali mtu kwa mtu nyumba kwa nyumba" Mhe. Subira Mgalu.

Baada ya hapa tarehe 20 Oktoba kutakuwa na mchakato ndani ya CCM sasa hapa ndio tunaendelea kuhamasisha wanawake kwa vijana tunatathimiwa, Ccm ina amini katika kugombea kuchaguliwa na kuchagua tujitokeze kuchukua fomu za kugombea. Kina mama na vijana msiogope.

Fomu moja tu ndio tumelipia ya Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Fomu ni za wote tukachukue tugombee ili mradi tufuate utaratibu.

Rai yangu ndani ya chama ni tuimarike vizuri tusigawanyike tusiwe na nongwa na viongozi katika chama mjipange vyema maana nyie ndiyo mnatuletea kongozi atakayeingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi" amesema Mhe. Mgalu.

IMG-20241013-WA0369.jpg

Katika muda wa kuwanadi wagombea ni wasihi wana kamati ya ushindi na Wanachama wote fanyeni kazi na kupangua hoja kwa yote yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, awamu hii amna kupita bila kupingwa, demokrasia imeimarishwa na sheria mpya za chama cha siasa zimetungwa hivyo tuseme maendeleo yaliofanywa ili tukisimamisha mgombea awe na nguvu kubwa ya ushawishi kupitia CCM" Amesema Mhe. Mgalu

Changamoto zipo na Serikali ipo kuzitatua katika kata hii ya Kerege nimpongeze Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa amefanya kazi kubwa ikiwemo kwa kuongeza jengo la mochwari, jengo la Mionzi (X-ray na Ultrasound). Bajeti ya ujenzi wa Wodi ya Watoto na Wanaume nimewasilisha Wizara ya afya na hivi punde tutegemee ujenzi wa wodi hizo kuanza" Mhe. Mgalu.

Aidha, Wanawake ni jeshi kubwa mwanamke mwenzetu anatutegemea sana tusimuangushe ameirudia tena historia ya mwanamke ambayo ilikuwepo wakati wa harakati za uhuru enzi za kina Bibi Titi Mohamed" Mhe. Mgalu.

Mwisho, Nawapongeza wote mlioshiriki katika ukarabati wa Ofisi zetu za Chama, natoa ahadi ya kutoa madirisha ya ofisi hii ili jengo liwe alama sahihi ya Chama chetu cha Mapinduzi na wakati wote kama kiongozi wenu nipo na tutazikushirikiana. Mhe. Mgalu.
 

Attachments

  • IMG-20241013-WA0367.jpg
    IMG-20241013-WA0367.jpg
    169.5 KB · Views: 2
  • IMG-20241013-WA0371.jpg
    IMG-20241013-WA0371.jpg
    162.5 KB · Views: 1
  • IMG-20241013-WA0372.jpg
    IMG-20241013-WA0372.jpg
    174.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom