Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE WA WAFANYAKAZI MHE. JANEJELLY NTATE AZUNGUMZA NA WATUMISHI OFISI YA RAS (KATIBU TAWALA MKOA) DAR ES SALAAM
Mbunge wa Viti Maalum Wafanyakazi Taifa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate leo tarehe 08 Machi, 2023 amezungumza na watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam kikao kilichohudhuriwa na Katibu Tawala (RAS) Dar es Salaam Bi. Rehema Seif Madenge.
Mhe. Ntate amemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na amesema; Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa miaka miwili aliyokaa madarakani kati ya masuala 16 ya wafanyakazi ametekeleza masuala 8 ambayo ni;
1. Kupanda vyeo (Promotion) - Miaka 6 bila Promotion kwa wafanyakazi
2. Madeni ya wafanyakazi;
3. Malimbikizo ya mishahara;
4. Nauli za kwenda likizo;
5. Malipo ya uhamisho;
6. Kupanda kwa mishahara ya wafanyakazi;
7. Kutoa Uhuru wa vyama vya wafanyakazi;
8. Kuelekeza mwaka wa fedha wa 2023/2024 watumishi waliofutiwa barua za kupanda madaraja 2016 na 2017 warejeshewe vyeo vyao walivyokuwa wamenyang'anywa
Mhe. Ntate amesema kila mapumziko ya Bunge huwa anaenda Mkoa mmoja kusikiliza shida, ushauri na maoni ya watumishi kwa mwamvuli wa TUCTA na kuzipeleka Bungeni kuzisemea.
Mhe. Ntate amesema Rais Mh.Dkt. Samia anawataka wafanyakazi wote kuwa waadirifu katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato, Manunuzi, utendaji wa weledi na uadilifu katika kazi, uaminifu na utiifu maana kwa kufanya hivyo maslahi yanaweza kupanda.
Mhe. Ntate amewatakia wanawake Siku njema ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na kupambana kupata haki za Wanawake na kuwahimiza kusimamia Kauli Mbiu: "Ubunifu na Mabadiriko ya Teknolojia katika Usawa wa Kijinsia"
Mhe. Ntate amemuomba Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam (RAS) kuwa tarehe 19 Machi, 2023 awaruhusu watumishi kushiriki sherehe za kumpongeza Rais Mh. Dkt.Samia kwa Miaka Miwili Madarakani zitakazofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Mhe. Ntate amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla kwa kusimamia vizuri usalama kwa kuondoa kundi la Panya road ambalo lilikuwa linahatarisha usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Naye katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam (RAS) Bi. Rehema Seif Madenge amemshukuru Mbunge Mhe. Ntate kwa kukutana na wafanyakazi kwni kwa kufanya hivyo kunawafanya watumishi kukumbuka wajibu wao na kusema kuwa amekuwa akiwa na utaratibu wa kuzungumza na watumishi hao mara kadhaa ili kukumbushana majukumu.
Solidarity Forever