samagi
Member
- Dec 26, 2017
- 53
- 34
Leo trh 26/12/2017 Imekuwa ni siku ya huzuni kwetu baada ya ndg Jeremiah Mrimi wa kijiji cha Kenokwi kata ya Mosongo Kuuwawa na Tembo usiku wa kuamkia Krismas. Huyu ni ndugu na Diwani wa kata ya mosongo Mh. Samson Mrimi.
Tembo kwa sasa ni tishio kwa uhai wa wananchi wa Serengeti, mamia ya watu wamekwisha angamizwa na Tembo , Pamoja na ahadi nyingi za serekali kujenga uzio kuzuia hawa wanyama kuvamia mashamba na makazi ya wananchi mpaka sasa hakuna dalili yeyote ya kutenga bajeti kuwazuia wanyama hawa.
Siku wananchi wa Serengeti wakiamua na wako mbioni kuamua hatima ya maisha yao dhidi ya Tembo ipo siku hao tembo wataisha.
Tumeshazika wanaserengeti wengi mno wala serekali haijali bali yenyewe inafurahia kukusanya mapato lkn kuwasaidia wanaserengeti imeshindikana kabisa.
Pamoja na Mimi kumwandikia spika wa bunge kuhusu tatizo la Tembo na spika kumtaka waziri wa maliasili kuchukua hatua , ambapo tulizuru maeneo yaliyoathirika na Tembo Mimi na waziri bado mpaka sasa wizara imeziba pamba masikio. Ok sawa hayo masikio ipo siku yatazibuliwa pale raia watakapoamua kuchukuwa hatua.
Njaa yao, mauwaji yao sababu ya Tembo? No No No inatosha.source mbunge mwenyewe