Pre GE2025 Mbunge Zaytun Swai Apita Mtaa kwa Mtaa Kuhamasisha Wananchi Kushiriki Uchanguzi

Pre GE2025 Mbunge Zaytun Swai Apita Mtaa kwa Mtaa Kuhamasisha Wananchi Kushiriki Uchanguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Mhe. Zaytun Seif Swai ameendelea na Ziara yake mkoani Arusha Kuhamasisha watu kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na kutembelea vituo vya huduma za Afya.

"Tumeendelea kuhamasisha Wananchi kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwezi Novemba mwaka huu ili kuchagua viongozi wenye sifa na wanaotokana na CCM ili waweze kuendeleza kazi nzuri iliyokwishafanywa na Rais wetu" - Mhe. Zaytun Seif Swai

Mbunge Zaytun Seif Swai ametoa Shukrani kwa Serikali ya CCM kwa kuboresha miundombinu na huduma za Afya katika Jiji la Arusha, kina Mama wanafurahia huduma nzuri zinazotolewa katika kituo cha Afya cha Mkonoo Kata ya Terati

Aidha, Zaytun Seif Swai amesema pamoja na maboresho makubwa ya miundombinu ya Afya, Serikali bado imeona umuhimu ya wagonjwa kulala sehemu safi na kumshukuru Rais Samia kwa zawadi ambayo kupitia Wabunge wameweza kuwasilisha kwenye vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali

Pia, Mbunge Zaytun Seif Swai ameendesha Mkutano wa kusikiliza changamoto za wananchi wa Tarafa ya Suye uliofanyika nyumbani kwa Balozi Shina Na 1 Wa Kimandolu Ndugu Raphael Nanga ambapo aliambatana na Wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi changamoto kwa haraka.

Akiwa nyumbani kwa Balozi Shina Namba 1. Kimandolu Ndugu Raphael Nanga, Mbunge Zaytun Seif Swai amegawa Bendera kwa Mabalozi wote ikiwa ni Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwezi Novemba mwaka 2024.

#ArushaYaKijani
#MbungeKazini!

WhatsApp Image 2024-08-01 at 19.03.13.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-01 at 18.42.10.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-01 at 18.41.15.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-01 at 18.39.07(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-08-01 at 18.39.07.jpeg
Screenshot 2024-08-01 at 17-59-38 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-58-37 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-57-39 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-57-15 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-56-50 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-56-00 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-55-36 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-54-49 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-54-31 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-54-16 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-08-01 at 17-53-06 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png
 
"Tumeendelea kuhamasisha Wananchi kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwezi Novemba mwaka huu ili kuchagua viongozi wenye sifa na wanaotokana na CCM ili waweze kuendeleza kazi nzuri iliyokwishafanywa na Rais wetu" - Mhe. Zaytun Seif Swai
Halafu wakishachagua?! What Next?
 
Viti maalum vifutwe tu
Hawa ni mzigo

Ova
 
Back
Top Bottom