Mbuyu Ulianza Kama Mchicha

Mbuyu Ulianza Kama Mchicha

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA

Hapa katika kiwanja hicho wazee wetu walipojenga ofisi ya African Association Mtaa wa New Street na Kariakoo kwa kujitolea kufanya kazi ya ujenzi kila siku ya Jumapili leo pamesimama ofisi ya fahari ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba Avenue.

Hebu fananisha jengo hili na jengo la African Association kama lilivyokuwa mwaka wa 1933 katika siku ya ufunguzi wake Mtaa wa New Street.

Fananisha pia na muonekano wa jengo hilo hilo la African Association siku kilipoasisiwa chama cha TANU mwaka wa 1954.

Fananisha tena na jengo lilojengwa na TANU kabla halijavunjwa kupisha jengo jipya la CCM lililopo hivi sasa.

1660934789768.jpeg
1660934877171.jpeg
1660934932670.jpeg
1660935153817.png


Majengo haya yote kufuatilia jengo la kwanza lililojengwa na viongozi na wanachama wa African Association lililofunguliwa na Gavana wa Tanganyika wa wakati ule Donald Cameron yana historia yake.

Historia hii leo haipo ndani ya jengo hili la kupendeza linalosimama Lumumba Avenue wala historia hii haipo nje yake.

Siku ile pale New Street ndani ya ofisi ya TAA katika chumba kimoja walipokuwa wamekaa Mzee John Rupia, Abdul na Ally Sykes na Julius Nyerere wakijadiliana kama muda umefika wa kuunda chama cha TANU ofisi ya TAA ilikuwa haina hata umeme na hiyo barabara ya mtaa iliyokuwa inapita hapo nje ilikuwa vumbi tupu.

Chumba kimoja katika ofisi hii ya TAA alikuwa amepanga Muhindi mmoja aliyekuwa dobi akifua na kupiga pasi nguo.

Nani anayejua historia hii ya hawa wazalendo wanne ambayo safari hii kwa Julius Nyerere ilianza mwaka wa 1953 katika ukumbi wa Arnautoglo ambako Nyerere aligombea nafasi ya rais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes?

Lakini mpaka lini sisi tutakuwa nchi ambayo haina historia yake hata ndani ya alama mfano wa majengo yanayoakisi juhudi za waliotutangulia kama utambulisho wetu?
 
Walau leo sijaona neno uislamu na kumtambua nyerere Kama mzalendo

Endelea hvhv mzee wangu

Picha hakuna
Peramiho,
Soma vizuri utuwaona Waislam.

Ni vigumu sana kuwatoa Waislam katika historia ya siasa ya Tanganyika.

Mfano wake ni kama vile kueleza historia ya Ujamaa Vijijini bila ya kumtaja Julius Nyerere.

Waliojaribu kuwaondoa Waislam katika historia ya uhuru ndiyo waiotufikisha hapa leo wewe unaisoma upya historia ya Julius Nyerere.
 
Back
Top Bottom