Mbuzi aina ya Isiolo/Gala, kondoo wa Black head au Doper na Mbuzi wa maziwa

Mbuzi aina ya Isiolo/Gala, kondoo wa Black head au Doper na Mbuzi wa maziwa

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Mbuzi wa aina ya Isiolo au Gala ni mbuzi weupe ba wenye maombo makubwa ni wazuri sana kwa ajili ya nyama na sanapatikana sana nchini Kenya.

Pia kuna Kondoo Black Head au Doper ambao asili yake ni South Africa, gawa ni kondoo wa nyama ni wakubwa sana, na hawa pia unaweza wapata nchini Kenta na pia Mbuzi wa Maziwa.

Hawa mifugo unaweza waingiza Tanzania kupitia Namanga au Tarakea na kwa kibali cha idara ya mifugo.

Ni mbegu nzuri sana za kuwa nazo shambani kwako.
View attachment 2320469View attachment 2320472View attachment 2320473View attachment 2320475View attachment 2320477
 
Namuelewa sana Dorper, huyu kondoo ana demand sana nchini Kenya. Kwa wanaoelewa, nyama yake ni tamu sana hata zaidi ya mbuzi. Kwa miaka kadha sasa nimekuwa nikitafuta dorper, kila mara wakati wa sherehe muhimu za kifamilia.

Yaani walishazoea kabisa na huwa wanauliza mapema kama dorper atachinjwa ndio waje mapema. 😄 Zamani walikuwa wanapenda nyama ya mbuzi na kuchukia sana ile ya kondoo. Dorper ni tofauti sana na kondoo wa kawaida.

Jamhuri dei iliyopita nilimnunua dorper mkubwa kama huyu hapo chini(black headed), kwa bei ya shilingi 14,000(KES). Ila ilibidi nisafiri hadi maeneo ya Illbisil, gatuzi la Kajiado karibu kabisa na mji wa Namanga kwenye highway ya Nairobi-Namanga. Wanafugwa sana kule.
11-600x465.png
 
Back
Top Bottom