Huko Vietnam Sasa vita ilikuwa imezidi kuwa mtihani mkubwa zaidi kijeshi kuikumba nchi hiyo kubwa zaidi kijeshi Kwa miongo kadhaa.
Vijana wa Kimarekani walikuwa wakiangamia vibaya sio kwasababu hawakuwa bora kivita, walikuwa bora zaidi lakini hapo Vietnam walikuwa wamekutana na watu wasio na mafunzo yoyote maalum ya kivita Bali watu wenye moyo uliopandikizwa vyema fikra za kizalendo Naam.
Mioyo hasa isioyumba Iko tayari kufa kuhakikisha kwamba utaifa, uhuru wao na utambulisho wao unadumishwa.Adui aliyewaingilia magetoni hakutakiwa kurudi salama nyumbani na hata akirudi nyumbani awe dhaifu afe Kwa majeraha.
Adui yao sasa alikuwa ni mmoja tu jeshi la Marekani lililojizatiti vyema katika ukanda ule wakiwa na madege bora ya kivita , magari bora, mafunzo bora bila kusahau melivita mamia Kwa mamia zote dhidi ya taifa dogo la Asia ya kati Kwa jina Vietnam.
Wamarekani na washirika wake walikuwa wameamua hata Kwa maguvu ya kijeshi wWavietnam lazima wapige goti, waombe poo na waukubali ubepari na kuacha kabisa evil system ya kiuchumi kama walivyoita wao yaani ukomunist kutoka Soviet Russia.
Kwa nguvu moja vijana, wazee, watoto, vikongwe na hata wanawake wakaungana kumpiga adui huyo. Unaambiwa haikuwa rahisi kumjua ni nani mpiganaji nani raia wa kawaida. Vita ikapamba moto Vietcong kikosi cha wanamgambo kutoka Kaskazini wakifadhiliwa na Sovieti wakawabananisha Wamarekani vilivyo hapo Wamarekani wakapigika hasa.
Mpaka mwaka wa 1962 Wamarekani walikuwa wamepoteza ndege vita zaidi ya 3000 bila kusahau askari maelfu Kwa maelfu. Wakiwa wamejizatiti Kwa silaha nzito za msaada kutoka Usoviet ndege vita Mig 21 state of the art ya kisoviet, ndege vita za Kimarekani f 4 zikapata shida kwelikweli huko angani, ardhini ndo usiseme Kila mtu alikuwa na Manpads zote kuhakikisha hakuna ndege ya maadui inafanya mashambulizi kirahisi hapa ndipo yalipotokea maanguko ya ndege za kisasa kabisa yaani B 52.
Dege hili la kutupa makombora mazito likaangamia hapo, huku chini maporini ndio usiseme ambush zikawarudisha watoto wa Kimarekani kwenye body bags.
Hali ilivozidi kuwa mbaya zaidi Wamarekani wakaamua kuja na kemikali maalum ya kuwafukunyua wavietcong huko kwenye misitu minene ama isitoshe wafe kwa sumu ya kemikali hii. Bila fikra za hatma ya jambo hili Wamarekani wakamwaga Lita maelfu katika misitu ya Vietnam. Hapa wakafa Wavietcong malaki inakadiriwa kuwa ni laki nne hivi.
Sasa basi kama nilivyosema mwanzo aidha Kwa mchecheto wa kipigo au kutokujua kemikali hii Sasa ikashindwa kutofautisha kati ya Wavietcong na askari wa Marekani. Ikawa kama vile tukose wote askari wao pia wakafa Kwa agent orange. Waliopona wakapatwa na magonjwa mazito kama uoni hafifu, kufeli Kwa Figo na mapafu hata leo.
Kutoka mwezi Januari mwaka 1968 mpaka mwaka wa 1971 karibu robo ya Vietnam ilikuwa imeathirika na kemikali hii.
Ajabu ni kwamba wote waliobaki wazima wagonjwa Kwa wazima wakaendelea kusimama kidete silaha mkononi dhidi ya mvamizi huyo aliyetoka maelfu ya kilomita aliyejitolea kuwafundisha wao kile kiitwacho demokrasia na ustaarabu. Tofauti na siku zilizopita jambo hili la agent Orange likachochea hasira zaidi kwa wananchi.
Hata wale waoga sana wakajisemea mioyoni inatosha hawa ni maadui wanatuulia wazazi, watoto, wazee bila kujali ni wapiganaji ama laah.
Watu wakaungana zaidi katika kipindi hiki Marekani akazidi kupoteza ndege vita zaidi, helicopter zaidi, rasilimali watu zaidi na Amored Personnel carrier zaidi.
Mh Kule Marekani napo kelele acheni vita zikazidi kuongezeka. Lakini laah taifa kubwa kama Marekani kuwakimbia wanamgambo itakuwa ni aibu kubwa. Hatuondoki wakaamua kuendelea kufa huko ugenini kuepusha aibu hii.
Ndipo Sasa katika hali hii ya kuishi bila matumaini ya kutokujua kama watakuwa hai sekunde mbili tatu zijazo vijana wa Kimarekani wakaanza kupoteza nidhamu, wakaanza kupoteza kujiamini, wakaanza kuathirika na msongo wa mawazo. Katika kundi hili la waliopoteza matumaini Kwa kuhofia ukatili vitani basi kulikuwa na kikundi kidogo maalum cha kiplatuni Chenye vijana 48 walioiva vizuri.
Platuni hii ilikuwa ikiongozwa na kijana mmoja mweupe wa Kimarekani, mwenye umri wa miaka chini ya 30. Alikuwa ni afisa na team leader wa Platuni hii. Kijana huyu baba na mama yake walipomkaribisha duniani hapo mwezi Juni mwaka 1948. Wakaamua kumuita jina la William Calley mtoto yule. Si mama Wala babaye waliojua njia na hatma na maisha ya mtoto yule ila mola mlezi.
William Calley akakua, akaanza shule na Sasa akaingia jeshini mnamo mwaka wa 1966 ili kupigania nchi na maslahi yake popote duniani. Dogo William akafuzu mafunzo maalum ya kijeshi akatupwa Vietnam akiwa na wenzake Bora kama yeye wapatao 47 hivi.
Vijana hao walioaminika walikuwa wametupwa hapo kufanya misheni nzito wakiwa wachache Kwa ufasaha zaidi. Moja ya missheni zao ilikuwa kunyang'anya silaha Kwa wavietcong, na kuhakikisha rescue mission za majeruhi.
Kwa morali Yao walitegemewa kufanya makubwa sana. Chaajabu , waswahili husema vita si lelemama vijana hawa wakaanza kufa mmojammoja Kwa mashambulizi ya namna za vita ya msituni kutoka Kwa Vietcong. Kutoka jumla Yao 48 walipofika hapo mwishoni mwaka wa 1968 Sasa huo ni mwaka 1969 walikuwa wamebaki 27 tu.
Si unajua Tena ujana ,urafiki wa kweli na namna ilivyo ngumu kuwapoteza marafiki zako wapendwa? Uchungu hasira, visasi na roho mbaya dhidi ya wauaji ikatawala mioyo michanga ya vijana hao.Naam hasira dhidi ya Vietcong. Wakajiapiza kwamba watapambana kishujaa kulipiza kisasi cha fallen heroes wa Platuni yao.
Hili jambo likawa moja sababu ya Calley na kikundi chake kufanya jambo la ovyo zaidi na fedheha Kwa jeshi hilo bora zaidi duniani. Je Lieutenant William Calley amefanya Nini?
Tafadhali endelea kusubiri.