Mbwa:Anaweza kuwa Mateka wa Kivita (POW) ?

mkada

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
1,200
Reaction score
907
Picha waliyoiweka kwenye akaunti yao (Wataliban) ya Twitter, inaonyesha Mbwa mdogo wa hudhurungi akiwa na kamba ndogo shingoni. Taliban wanasema kuwa Mbwa huyo kwa jina, 'Kanali' alikamatwa usiku wakati wa msako uliofanywa mwezi Disemba. Mbwa huyo alikuwa na tochi ndogo, kamera na kifaa cha GPS.

Pia walionyesha silaha walizonasa wakati wa msako huo, ambazo hutumiwa na kikosi maalum cha jeshi la Marekani. Mwandishi wa BBC anasema kuwa kumekuwa na taarifa za kiongozi wa Taliban katika eneo hilo kuonekana akiwa na Mbwa huyo ambaye sasa ni mfungwa wa kivita.

Source:BBC

Swali kwa wataalamu wa International Humanitarian Law, Je, mbwa anaweza kuwa mateka wa kivita, na akapewa stahili na haki zote kama mateka wa kivita wa kawaida na nchi iliyomkamata??


 
hao matalibani sio siri wanalaana pamoja na radi
 
Walijuaje jina la huyo mbwa?
Au walimuuliza!
 
Katika shule yangu ya humanitarian law sikuwai kuona kama mmnyama (mbwa) anastatus ya combatant kwenye battle field...ngoja nifungue madesa I will be back
 

Hiyo hapo juu ni article 4 ya Geneva convention kuhusu wafungwa wa kivita(POWs)

Natumai itakusaidia
 
Ukishasema Humantarian Law its obvious haiwez kukupa jibu la kiumbe kama Mbwa cz yenyewe imespecialize kwenye "Human" as the word Humantarian was derived from a word "human".
POWs utapata status yao vzur kwenye Geneva convention na Marshall law. Mbwa anaweza kua POW kama atakua member wa combat unit mfano cairo aliyeshiriki Operation Neptune Spear against bin Laden had a Military rank so ni member wa Armed forces.
As a member of armed forces mbwa akifa huzikwa kwa heshima zote za kijeshi kama mwanadamu wa kawaida na pia hupata Military promotion wanapofanya "act of velor" mfano Cairo alitunikiwa nishani ya ushujaa na Obama alingside other SEALs Commanders.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…