Mbwa huyu ni chotara wa aina gani?

Mvumbo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
3,489
Reaction score
12,137
Habari wakuu,
Kwa wale wajuzi wa aina za mbwa naomba mnisaidie utaalamu wenu kwa mbwa huyu, anaonekana ni chotara sasa ndio nataka kuelewa amechanganyia na mbwa gani kwa muonekano wake. Ana mkia mfupi na mnene na kifua kipana.

 
Mbwa wa kawaida tu kama mbwa wengine.
 
Mbwa mwitu wana mikia mifupi na minene na masikio kama ya bobby hapo juu.
 
Hamna kitu sipendi kuona mbwa kafungwa kamba shingoni kama mbuzi

atleast mtu atumie nyororo ila hata nyororo pia sipendi sana

kwanini mbwa asipelekwe bandani kwake au kwann asitengenezewe sehemu yake

kisha akaachwa huru?
Nikweli Mbwa hafungwi kwa kamba ya katani, lakini tena tunashauri Mbwa asikae sana bandani nao ni wanyama ambao kunawakati wanahitaji uhuru wao na kuzunguka eneo la nyumba, hii huwasaidia Mbwa kutoa stress zakufungiwa mno. Unaweza ona Mbwa anafoka kila saa akiwa bandani ukafikiri ni mkali kumbe ni stress za kufungiwa kila mara
 
Sahihi kabisa ila kama ni wa ulinzi anatakiwa asionane sana na watu.
 
Mbona mpole Sana Huyo mbwa..au Ni chotara aliyechanganyika na mbuzi
Mbwa hatari sana huyu zaidi ya unavyodhani, mbele yake hakukatizi kiumbe chochote kabla hajakitoa damu hususan binadamu.
 
Hamna kitu sipendi kuona mbwa kafungwa kamba shingoni kama mbuzi

atleast mtu atumie nyororo ila hata nyororo pia sipendi sana

kwanini mbwa asipelekwe bandani kwake au kwann asitengenezewe sehemu yake

kisha akaachwa huru?
Ukifungua banda tu power anayotoka nayo hakuna wa kumzuia na hudhuru chochote atakacho kutana nacho.
 
Sahihi kabisa ila kama ni wa ulinzi anatakiwa asionane sana na watu.
/Quk
Ukali wa Mbwa unategemeana na koo aliyotoka na vile atakavyo fundishwa, kumfungia ndani tuu sio njia sahihi ya kuleta ukali kwa Mbwa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…