Mbwa kala mbwa

Mtuache

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
256
Reaction score
658
Mwanamke mmoja aliamua kusherehekea siku yake ya kutimiza miaka sabini duniani kwa kwenda kulala katika hoteli moja nzuri. Wakati anaondoka asubuhi mhudumu akampatia bili ya shilingi laki tano.

Akahitaji kujua kwa nini bili ni kubwa kiasi hicho kwa kusema, "Nakubali hoteli yenu ni nzuri lakini vyumba havina thamani ya laki tano kwa kulala usiku mmoja tu ukizingatia hata chai sijanywa."

Mhudumu akamwambia hiyo ni gharama ya kawaida na kama angelihitaji chai basi angelipatiwa.

Hakukubali. Akaomba azungumze na meneja.

Mhudumu alimwita meneja na alipokuja akamweleza hali nzima ilivyo. Meneja akasema, "Hii hoteli ina bwawa la kuogelea linalokidhi viwango vya olimpiki na ukumbi mkubwa wa mikutano ambayo ungeweza kuitumia."

"Lakini sikuitumia." Mwanamke alijibu.

"Vyema. Vipo hapa na ungeliweza kuvitumia."

Meneja akaendelea kumwambia mteja kuwa angeliweza kutazama burudani mbalimbali mashuhuri ambazo hufanyika hapo hotelini.

"Tuna watumbuizaji kutoka dunia nzima wanasherehesha hapa."

"Lakini sikwenda kuwatazama."

"Vyema. Tunao na ungeliweza kwenda kuwatazama."

Kila alichokitaja meneja kutetea bili ya hoteli, jibu la mwanamke liliendelea kuwa moja tu, "Lakini sikutumia" na meneja akawa anatamba kwa kumwambia, "Kipo hapa na ungeliweza kukitumia."

Baada ya dakika kadhaa za vuta n'kuvute na meneja akiendeleza msimamo wake mwanamke akakubali kulipa. Aliandika cheque na kumpatia meneja.

Meneja alipigwa bumbuwazi baada ya kuitazama cheque. Akamwambia mteja, "Mama tunayokudai ni laki tano. Mbona kwenye cheki umeandika laki pekee."

"Uko sahihi. Laki nne ni gharama ya kulala na mimi."

"Lakini sijalala na wewe." Meneja alitamka macho yamemtoka.

"Vyema." Mwanamke alijibu kisha akamalizia, "Hilo ni tatizo lako kwa sababu nilikuwa hapa na ungeliweza kulala na mimi."
 
Ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaa
Toba mbavu zanzgu jamaniiiiiiiiiiiiiii
Hiiiii kali
 
Kweli mbwa kala mbwa Hahahahahaaaaaaaa πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…