Mbwa kujisalimisha kwa chatu

Mbwa kujisalimisha kwa chatu

Ofsa Kidali

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2021
Posts
212
Reaction score
119
Habari za muda huu wakuu, hongereni kwa mapambano ya usiku na mchana kuendelea kuifanya nchi yetu na dunia kwa ujumla kuwa sehemu bora na salama.

Iko hivi, nina mpango wa kufuga mbwa shambani kwa sababu sio siku nyingi nitaweka mifugo mingi kiasi lakini bado hakuna uzio(fence), sasa kuna jamaa yangu kaniambia kwamba nitakachokifanya itakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu kwani mbwa huwa wana kawaida ya kujisalimisha wenyewe kwa chatu kwa ajili ya kumezwa(kuna vichaka vingi na vikubwa maeneo yanayolizunguka shamba). Hii ina ukweli wowote?

Kama ishu ni aina ya mbwa na mafunzo ni kwamba ninafikiria kati ya boerboel, GS au Doberman pinscher na nitawagharamiamafunzo.

Ushauri wenu tafadhali 🙏.
 
Habari za muda huu wakuu, hongereni kwa mapambano ya usiku na mchana kuendelea kuifanya nchi yetu na dunia kwa ujumla kuwa sehemu bora na salama.
Hizo ni Story za Vijiwe vya Kahawa, Iko hivi Mbwa hajisalimishi kwa Chatu Bali huwa wanaenda kumshangaa chatu hasa Magamba yake, na pale kama Chatu ana njaa basi hukamata mmoja, Hata nyoka wa kawaida mbwa ana tabia ya kwenda kumnusa nusa na hicho ndio kinacho tokea kwa Chatu pia.

Mbwa mwitu wao wana mafunzo ya asili wakimuoana Chatu tiyari wanajua ni adui na hawawezi enda kunusa nusa.

Kama eneo ulipo lina Chatu na una Mwmbwa siku una muona Chatu ita Mbwa wako, then angalia wanacho fanya, wataenda Direct kuanza kumnusa nusa na huwa hawajui kama yule ni adui na anaweza wameza,
 
Habari kama hizi Mimi pia nimekuwa nikizisikia.

Hizi ni miongoni wa taarifa ambazo huwa tunarithishana Vizazi na Vizazi bila hata kuwiwa kutafuta ni nini haswa kinatokea....utasikia Mtu anakuhadithia habari za Vibwengo, ukimuuliza umewahi kuwaona anakwambia amehadithiwa...na utatafuta mpaka uchoke hutompata aliyewahi kukutana na hao Vibwengo.

Nadhani Mchangiaji mmoja hapo katoa maelezo mazuri ambayo walau yanadhihirisha kuwa kuna Watu wamefanya utafiti na kujua kinachomkuta Mbwa, na si Mbwa tu bali Wanyama wengi wenye tabia ya kudadisi.

Na kama anavyoelezea Mchangiaji hapo Mimi kwa upande wangu nilitafuta taarifa nikakuta ni kwamba Mbwa huvutiwa na harufu inayotoka kwa Chatu, hivyo inapelekea kumsogelea akidhani inaweza kuwa ni chakula...Pia ukumbuke kuwa Nyoka wengi wana uwezo wa kutulia sehemu moja bila kujitikisa tofauti na viumbe wengine walivyo, maana hata namna yao ya kujilinda hufanyika wakiwa wametulia sehemu moja...hivyo ni rahisi kumvutia Mnyama Mwingine hata kama sio Mbwa kushawishika kumsogelea kujiridhisha kama yule ni Kiumbe hai au ni Mzoga.

Na si kwamba Chatu atammeza tu Kiumbe wake ghafla, la hasha Chatu hulazimika "kumkwida" Kiumbe husika mpaka atakapojiridhisha kuwa sasa anaweza kumeza bila Kiumbe husika kujitetea...na hawezi kufanya hivyo mpaka awe karibu na Windo lake, kwa Windo lenyewe kumkaribia au Yeye kumkaribia...na rahisi kwake ni yeye kukaribiwa kuliko kufuata.
 
Kuna wengine wanasemaga ukihisi harufu ya viazi kwenye kichaka basi ujue hiko kichaka kina chatu 😂😂

Shikamoo vijiwe vya kahawa 🙌

Hiyo yawezekana ni kweli, lakini mimi na hakika juu ya nyoka aina ya moma (puff adder) ukisikia/kunusa harufu ya wali, hiyo ndio njia yake ya kuvutia mawindo kama panya nk.
 
Ukiacha harufu tatizo ni kwamba mboni za macho ya mbwa zikiangaliana na mboni za macho ya chatu mbwa hulegea na hawezi kuondoka, ila mtu akimrushia kitu kama jiwe na kumpiga huyo mbwa ata shtuka na kuondoa macho kwa chatu na kukimbia. Tuwe na utamaduni wa kutembelea snake park zetu tutajifunza mengi sana.
 
Ukiacha harufu tatizo ni kwamba mboni za macho ya mbwa zikiangaliana na mboni za macho ya chatu mbwa hulegea na hawezi kuondoka, ila mtu akimrushia kitu kama jiwe na kumpiga huyo mbwa ata shtuka na kuondoa macho kwa chatu na kukimbia. Tuwe na utamaduni wa kutembelea snake park zetu tutajifunza mengi sana.
na hii haijalishi kama ni mchana ama usiku?
 
Back
Top Bottom