Mwanzo, hatukuwatambua tulijua ni washirika wenzetu wazuri tunaosafiri kwenye safina moja kuelekea nchi ya maziwa na asali, Kaanani yetu. Kwa jinsi walivyokuwa wanasifu na kuabudu pamoja na kupanda kwenye madhabahu mbalimbali kutoa mahubiri ya kutujaza imani, kweli tulijua ni kondoo wazuri wasio na madoa.
Kumbe wapi bwana, duuh tangu aliyejuu kumtwaa mchugaji kiongozi aliyefananishwa na masihi Yesu Kristo tumegundua kumbe washirika hawa ni mbwa mwitu wakali waliokuwa wamevaa sura ya kondoo.
Mbaya zaidi tunaambiwa washirika hawa pasipo soni wengine walishiriki kwenye dhambi iliyomlazimu Mungu kushuka duniani na kuchoma miji ya sodoma na gomora, tunaelezwa ni wabobezi kwa ubakaji kwa dada zetu haswa warembo kama Absolum mtoto wa mfalme Daudi.
Wengine walijiingiza kwenye unyang'anyi, uporaji na utoza ushuru wa mabavu, kwa kivuli tunaingia uchumi wa kati. Cha kushangaza zaidi Mchugaji huyo kiongozi alipopelekewa malalamiko alijibu kwa ukatili yeye hapangiwi na mshirika. Aliwapenda na kuwakasimisha madaraka makubwa yaliyowazidi uwezo wao.
Leo hii hawa Mbwa mwitu ni matajiri wakubwa wa kutisha ukwasi wao hauezeki , akaunti zao zimenona kwa unyonyaji waliofafanyia washirika wenzao, wameshiba kama kupe wakati kondoo wengine wamekondea sana kama vile hawana malisho. Hakika hawa wanastahili kusulubishwa tena kwenye misalaba yao iwe na misumari kutokana na dhambi walizotufanyia.