Idimulwa
JF-Expert Member
- May 27, 2011
- 4,944
- 2,459
UPDATES
KUHUSU KOMBO MBWANA TWAHA,GEREZA LA MAWENI TANGA.
Timu ya mawakili waliopiga kambi Jijini Tanga ikiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Wakili Michael Lugina na Wakili Deogratius Mahinyila katika kesi ya Jinai namba 000019759 ya mwaka 2024 ya Jamuhuri dhidi ya Kombo Mbwana Twaha.
Leo tarehe 18 july 2024 baada ya kukamilisha taratibu za dhamana kama ilivyo amriwa na mahakama siku ya tarehe 16 July 2024.
Walienda mahakama ya Hakimu mkazi Tanga kuonana na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Moses Maroa kwa ajili ya kufanya taratibu za dhamana na kupata amri ya Mahakama ya kumtoa gerezani Kombo Mbwana Twaha (Removal order) baada ya kutimiza masharti yake yote.
Mawakili wetu walinyimwa ushirikiano na Mheshimiwa Hakimu Moses Maroa.lakini tunashukru Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kwa kuingilia kati swala hili.
Tuna amini Mahakama kuu Kanda ya Tanga itamsimamia vyema Hakimu Mkazi Mwandamizi Tanga kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na siyo shinikizo lolote kutoka kwa yetote
kabla Jamii haijaijumuisha Mahakama ya Tanzania kwa ujumla wake katika kundi la Watesi wa Kombo.
Mawakili wetu wameelekezwa na Mahakama kuu Kanda ya Tanga kurudi tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kuonana na Mheshimiwa Moses Maroa kesho asubuhi kwa taratibu za dhamana.
N.B
1.Ikumbukwe Kombo Mbwana Twaha alisomewa mashitaka yake kwa siri bila uwepo wa Mawakili wake na nje ya muda wa Mahakama na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Moses Maroa
Kisha Kombo akakosa dhamana kwa sababu hakuna mtu wa karibu yake aliyejua kuhusu kufunguliwa kwa kesi hiyo. na mshitakiwa kupelekwa gereza la Maweni,Tanga muda wa usiku.
2.Jopo la Mawakili kutoka kona zote za Tanzania wamefungua kesi Mahakama kuu Kanda ya Tanga dhidi ya IGP,DPP na RPC Mkoa wa Tanga kwa kosa la kumshikilia Kombo Mbwana Twaha kwa siku 30 kinyume na sheria za nchi.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Happiness Ndesamburo siku ya tarehe 23 July 2024.
Mawakili waliojitokeza katika kesi hii mpaka sasa ni 1.Mpare Mpoki 2.Jebra Kambole 3. Hekima Mwasipu 4.Peter Madeleka 5.John Seka 6.Boniface Mwabukusi 7.Daimu Khalfani 8.Paul Kisabo 9.Fulgence Massawe na 10.Ferdinand Makore.
Chanzo: Salumu FB Page
Pia soma:Boniface Jacob: Habari mbaya kuhusu Kombo Mbwana Twaha