Mbwana Samata arejea kwenye ubora wake.

Mbwana Samata arejea kwenye ubora wake.

pangalashaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Posts
1,301
Reaction score
1,579
Mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Mbwana Samata anayecheza soka la kulipwa nchini Belgium emerejea katika ubora wake baada ya leo hii kuifungia magoli mawili timu yake ya Genk dhidi ya Sporting Charleroi katika ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama First Division A. Timu ya Genk ukiibuka washindi kwenye mechi hiyo kwa magoli manne kwa moja dhidi ya wapinzani wao. Mbwana alifanya goli la kwanza dakika ya 24 na goli la tatu dakika ya 61. Hili limekuja siku mbili baada ya Samata kuifungia timu yake ya Genk goli moja dhidi ya timu ya Gent ambapo timu hizo zilitoka sare ya goli moja moja, mchezo uliochezwa tarehe 10 mwezi huu wa May. Hizi ni habari njema kwa waenda maendeleo ya soka na washabiki wa Samata hapa nchini. Lakini pia ni habari mbaya kwa member mmoja humu, kwani siku chache zilizita alileta uzi humu JF akimponda Samagoal bila kufahamu kwamba alikuwa majeruhi kwa muda kidogo. Viva Samagoal!!!!!!!!
 
Mwacheni Samata. Hashim,basketballer,mlimvimbisha kichwa hadi akapotea.
 
Back
Top Bottom