Mbwana Samatta asaini rasmi Genk ya Ubelgiji

Wadau mbona naskia anaenda standard liege
 
Mbona Naskia TB mazembe wanambania na wanadai Mkataba wake unaisha January next year
 
Mshambuliaji wa tp mazembe atajiunga na KRC GENK ya ubelgiji baada ya timu hiyo kumnunua kwa yuro milioni 2.5 sawa na karibu billion 6 za kitanzani

SIMBA pia itanufaika na mauzo hayo kwa kua kwenye mkataba kiliwekwa kifungu
Safi sana naona ni njia ya wengne kukufuata i min mlango hao wanaovuta bangi wanze kujitambua na cyo waendkeze bangi
 
safi sana hayo ndo maamuz magumu nilikua nasubiria mazembe walikua hawataki kabisa asepe angebaki asinge tusua tena safi sana samata umeona mbali
 
Katumbi ni mtu wa pili kwa umaarufu na nguvu
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Anazidiwa kwa kiasi kidogo sana na Rais wa
nchi hiyo Joseph Kabila. Lakini upande
anaoupenda yeye sio siasa sana, ni muumini
mkubwa wa biashara. Kila anachokiona kwake
anakitazama kwa upande wa faida yake.
Kikimlipa anakipenda kwa moyo wake wote,
anakithamini kisha anakitunza, baadae mapenzi
yanazidi na anashindwa kukiachia.
Bahati mbaya sasa kahamia katika rasilimali
watu. Anamiliki timu kisha anamiliki wachezaji
wake. Anawalea wanavyotaka, anawapa ufalme
kisha anawafanya matajiri. Ukishakuwa nyota
anakufanya jirani yake, anakulipa kwa kila goli
unalofunga kisha anakufanya uamini kuwa kuna
maisha mazuri sana nje ya Florentino Perez.
Anakupa uhakika wa kuishi kifahari kuliko
wachezaji wengi wanaocheza ligi kuu ya
Ufaransa.
Bahati nzuri yeye hana maisha ya
Johannesburg, hana maisha ya soka la ndani.
Anapenda kuwafanya Waarabu waamini kuna
ushindani nje ya kule Kaskazini kisha anashinda
ubingwa wa klabu bingwa Afrika. Anakupa
uhakika wa kubadilishana jezi na Messi mwezi
December kwenye klabu bingwa dunia. Unapata
kiburi cha Mputu, umaarufu wa Kidiaba kwa
sababu ya pochi yake nene.
Pochi yake haijawahi kuwa tatizo kwangu.
Sijawahi kukwazika na ununuzi wake wa ndege.
Wakati anajenga uwanja wa thamani ya paundi
milioni 35 nilitambua fika aliamua kuweka
mabadiliko kwenye soka la Afrika. Alifanya
uwekezaji ambao ni rahisi kufanyika katika klabu
kongwe za Simba na Yanga kipindi ambacho
shabiki wa Tanzania atajua tofauti ya soka la
mapenzi na soka la uwekezaji.
Tatizo kwa Katumbi na mimi ni kalamu yake tu.
Kalamu yake ina akili sawa na medulla yake.
Kalamu yake haijawahi kwenda kinyume na
yeye. Kila wino unaodondoka kutoka kwenye
mdomo wa kalamu hiyo unazungumza vitu vipi
tu, TP Mazembe na Moise Katumbi. Ni kalamu
hii ndiyo ilimrejesha Patou Kabangu kutoka
Anderlecht mpaka TP Mazembe.
Ni kalamu hii iliyotaka kukwamisha usajili wa
Alain Dioko Kaluyituka kuelekea katika klabu ya
AL Ahly Doha ya Qatar. Ni kama ambavyo
kalamu hii inanipa hisia kuwa inataka
kumlambisha ardhi mchezaji Mbwana Samatta
maarufu kama Samagoal kwa wakongo. Kalamu
hii ishanusa upande wa pili wa karatasi za
Samatta. Inataka kuangusha wino ambao
imezoea kuangusha. Wino wa kumfunga
mchezaji au wa kumpa faida anayeimiliki Moise
Katumbi. Wakati watanzania wakiwa na furaha,
Katumbi amenuna. Amenuna hasa.
Samatta alishaamua hatobaki Mazembe.
Samatta alishaamua kuikwepa pochi nene ya
Katumbi. Maisha yake ya soka alishajua
yanavuka mipaka ya Afrika. Kipaji chake
maridhawa alihitaji kiwe jirani na Aubameyang.
Wakati Samatta anapanga yote haya, Katumbi
alikuwa kalala amekumbatia kalamu yake
maridadi. Akaifuata kalenda akagundua Samata
alikuwa hana zaidi ya miezi sita kwenye
mkataba wake.
Akasubiri kujua nini kitatokea. Akaivaa akili yake
iliyomfanya kuwa milionea akavua upenzi wa
soka. Kwake yeye kwa sasa alihitaji mikono ya
Samatta kuliko miguu yake tena. Genk
walivyogonga hodi Samatta akawakaribisha
kama tu ilivyo katika maandishi kuwa bisheni
hodi nanyi mtafunguliwa.
Kipindi hiki alijua FIFA na CAF wanamruhusu
kabisa kuzungumza na klabu yoyote anayoitaka
hata ikiwa ni kimondo ya Mwashiuya. Akasaini
mkataba wa awali na akawang’ata sikio Genk
kuwa harudi Mazembe. Genk kama ilivyokuwa
vilabu vinavyojielewa vya kimataifa vikaomba
kukutana na Mazembe. Katumbi akawepo
ambaye ndiye Mazembe yenyewe, wakamwomba
kumchukua Samatta mwezi Januari.
Katumbi kama mshambuliaji bora wa kibiashara
akavaa kalamu yake, akawaonesha Genk medali
za Samata, akawaonesha nyimbo anazoimbiwa,
pesa anayolipwa kisha akawaletea video za
mitaani pindi Samata anapopita. Akamalizia kwa
kuwaambia mfalme anaondoka kwa Euro million
2.5. Waliposita akashuka mpaka million 1
waliposita tena akang’ata kalamu yake,
akawaambia wazungumze.
Wao kwa kutambua watampata bure dirisha la
kiangazi wakasema wanatoa Euro laki 7.
Katumbi akavaa kofia yake, akaificha kalamu
yake kisha akawaacha na kahawa zao mezani.
Inasemekana mawazo ya utulivu hupatikana
bafuni. Akakumbuka kuwa tofauti na kalamu
kuna pochi nene kwenye mifuko ya nyuma ya
suruali. Akatuma mwakilishi kwa Samatta, kisha
akawawahi Genk kabla kahawa haijaisha.
Akaja na mbinu za Simba na Singano, akasema
Samata aliongeza mkataba wa mwaka mmoja
mpaka 2017. Genk wakacheza mchezo wa
chess yeye akacheza draft, michezo ya
kuviziana huku unawaza sana. Alipogeuka
nyuma akapata ujumbe mfupi wa salamu kutoka
kwa rafiki yake wa klabu ya Standard Liege.
Akaondoka zake na hotel aliyokuwamo akarejea
kwake. Akamtambulisha kijana kwa Standard
Liege, wakamtamani na wakakubaliana na dili la
kalamu yake.
Tatizo ni Samatta kuvunja mkataba wa awali na
Genk. Tatizo lingine likawa ni wapi Samatta
anapataka. Katumbi yupo tayari kugombana na
Samatta ili kalamu ifanye kazi yake. Hii ni tabia
ya matajiri wengi sana, kalamu huwa na
umuhimu kuliko pochi. Wino wenye sahihi huwa
mwamuzi wa mwisho.
Bahati nzuri ya Samatta ni kuwa mkataba wake
unamweka Katumbi katika ugumu. Ingawa
Samatta kashika mpini lakini Katumbi hajajali
kushika makali, kwake kwa sasa anahitaji sahihi
ya Samatta kuliko magoli yake ya baadae.
Anataka kupata pesa ya kuleta akina Rodger
Asale wengine huku akiongeza uwanja wa
mazoezi.
Wakati Samata pengine akiingia kwenye
harakati za Che Guevara bado napata shaka na
akina Ulimwengu na wanaomfuata Katumbi,
Ubwa na Chanongo. Napata shaka kama
wanajua kutofautisha kati ya pochi yake na
kalamu yake. Kalamu iliyowalaza pale Mazembe
Kalaba na Singuruma.
Wakati nikikumbuka akili za wachezaji wetu
katika sakata la kalamu za matajiri mwili
unanisisimka. Nikimkumbuka Mwashiuya au
Singano, machozi yananitoka. Natamani tupate
darasa la namna ya kushika kalamu. Acha
nianze na Ulimwengu, kaka ni sahihi wewe
kuitumia pochi ya Katumbi lakini usiitamani
kalamu yake. Ukikosea tu, Ufaransa itakuwa
umbali wa sayari ya Pluto.
 
Kama wachezaji wa tp mazembe hawajasoma kilicho mkuta mputu basi hawawezi kusoma tena.
 
Tafadhali tuhabarishe mkuu.Kipi kilichomkuta Mputu ambacho ni muhimu kwa wachezaji wa TP Mazembe kujifunza kwacho?.
Mputu alilelewa kama mfalme mazembe hakujishughulisha kuangalia mustakbali wa soka lake nje ya bara la african na uwezo alikuwa nao akadeka na kudhani mazembe ni mwisho wa soka lake leo yupo Angola huko.
 
Samata ndio mchezaji bora wa afrika kwa wachezaji wanaocheza league za ndani Jana alitwaa tuzo hiyo
Krc Genk ndio wanammiliki hivi sasa
 
Huyu yusuph soka kama ni kipaji halisi cha soka,atafutwe alipo asaidiwe,mnona kluvert alitolewa jela na rais ilihali ana tuhuma za ubakaji alikuwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…