Mbwana Samatta cheza mpira sasa

Agreed !
Tena asali sana pia maana huu umri anaosema anao ukipiga hesabu alipokuwa Lyoni na Simba data zinagongana !!

Mkuu nakubaliana na wewe tena kwa 100% kuwa Waafrika wengi hasa WACHEZAJI mpira hupenda KUDANGANYA kuhusu UMRI wao ila kwa umri wa Mbwana Samatta HAJAONGOPA mkuu amini usiamini ila tatizo kubwa la sisi Waafrika na labda niseme kwetu hapa Tanzania huwa hatufanyi Scouting nzuri kwa Wachezaji wetu na kibaya zaidi hatuzingatii hata DOCUMENTATION. Kwa mfano nenda pale TFF sasa hivi uliza jambo tu la mwaka 1985 au 1990 ukilikuta ni MSALIA MTUME. Mbwana nisiwe mwongo bado ni mdogo na hata huo UMRI wake ni sahihi nenda kokote kaulize isipokuwa kuna Wachezaji leo naambiwa bado wadogo mfano Nahodha wa Mtibwa Shaaban Nditi nasikia hata katika Passport yake imeandikwa NJEMBA ndiyo kwanza Inagonga 26 sasa tizama NYAGO lake ongeza na UNYUMBULIFU wake uwanjani kisha JIONGEZE.
 
Mtoa mada ushauri wako ni mzuri sana,Samata ameingia kwenye level nyingine ya Soka,anatakiwa ajikite zaidi kwenye kilichompeleka,Akiperform vizuri media zenyewe ndio zitamtafuta na kumpiga picha kwenye kila movement yake badala ya sasa yeye ndio anazitumia blog picha zake kama mleta mada alivyosema,

huwezi mlinganisha Samata na wanachokifanya kina Messi,Ronaldo au Benzema! wale wanacheza soka la Ulaya miaka kibao na wanalijua,pia wapo level nyingine sio level ya Samata,

tatizo humu jf kuna watu huwa wanafuata mkumbo tu,mtu mmoja hasa mtoa comment wa mwanzo kabisa akiiponda mada basi wengine hutiritika nao kuponda tu kwa kufuata mkumbo! Mtoa mada ushauri wako umemlenga Samata na nina imani akiupata atautafakari na kujitafakari,hawa wanaokukejeli wala wasikuvunje moyo,kama kweli ungekuwa unamuonea wivu Samata ungewezaje kumshauri vitu vyenye manufaa kwake?

Kumbukeni Samata ni kama analiwakilisha taifa so kumshauri ni vizuri na sio kitu kibaya.
 
Mbona ozil huwa anapiga picha miguu yake ikiwa na soksi huku anacheza game ya mpira geto kwake af anakula malike millioni, makoment laki9, mbona fresh tu.

Hapo hapo na mimi nakuomba mkuu fananisha makuzi na malezi ya Kisoka ya Mesut Ozil wa nchini Ujerumani ( ULAYA ) katika mji maarufu wa Munich na makuzi na malezi ya Kisoka ya Mbwana Samatta wa nchini Tanzania ( AFRIKA ) katika kitongoji maarufu cha Mbagala na Kimbangulile kisha urudi unipe TATHMINI yako.
 

We zitakuwa zimekuruka unalinganisha mchezaji wa real madrid na Genk ambayo kwa ulaya ni timu ya kawaida...
 


Heeee
 

Mkuu kwa HIKI KITU CHA MAANA NA KIZURI ULICHOKIANDIKA AMBACHO KIMENIFANYA SASA NIAMINI KUWA KUMBE WENYE AKILI NA UWEZO WA KUCHAMBUA MAMBO NA KUJENGA HOJA TUMEBAKI WACHACHE SASA. Nimekukubali sana mkuu, asante na naomba niseme tu kwako SHIKAMOO.
 
We zitakuwa zimekuruka unalinganisha mchezaji wa real madrid na Genk ambayo kwa ulaya ni timu ya kawaida...

Mkuu tena amerukwa sana tu msamehe. Vipi jana ulitia maguu darasani MSIMBAZI CENTER ambapo Father Xavier alikuwa anatoa pindi lake la Foundation of ETHICS? Halafu wadau wanakuulizia sana na umetususa mno. Nisalimie hapo Tigo GEREZANI, Mkeo na Mwanao.
 
Naona unaanzisha Uzi kwa ID moja then unakuja na IDs nyingine kujijibu na kujisifia.
 


Mkuu inawezekana una point nzuri sana

Ila una tatizo la kutotaka changamoto hakuna taaluma yoyote iliyowahi kupokelewa bila kupewa changamoto na madhaifu sembuse mawazo ya mtu mmoja?!

Labda ukubali pale mtu anapoichallenges hoja yako hata kama ni kwa pumba ijibu possitive unless otherwise labda wewe ni Le Mutuz uanze kublock kila anayekuchalenge kitu ambacho ni upuuuuzi!
 
We zitakuwa zimekuruka unalinganisha mchezaji wa real madrid na Genk ambayo kwa ulaya ni timu ya kawaida...
Wachezaji wa Madrid wanatumia matak.o kucheza mpira! Kama ni miguu majukumu yao ni yale yale na kujitumia ndio kunapelekea mtu kusonga mbele au kushindwa. Ricardo Kaka kacheza Madrid bado aliangukia pua japo hakuwa na mbwembwe, so soka au mchezo wowote ule hauondoi interests za mtu za nje ya uwanja na kama ukijituma na kuwa na displine utafanya vizuri tu. Huwezi lazimisha watu waishi kwa maono yako
 
Naona unaanzisha Uzi kwa ID moja then unakuja na IDs nyingine kujijibu na kujisifia.
Acha kuwa na fikra za kizamani,nimechangia kama member wa jf,kama wewe ulitaka member wote wa jf wampinge mleta mada hilo litakuwa ni tatizo lako binafsi kwa mleta mada.
 

Cha msingi hapa utujuze kiini ya sredi yako ni nini, maana umeto onyo bila kusema tatizo liko wapi, mtu huishi maisha kadri yanavomuijia., kwa mtu kama samata, mahali alipofika si kwamba alikua anakontroliwa, kafika kwa utashi wake.
 
Mkuu umeongea kitu cha maana sana! Natamani wote wale wanaopenda kuanzisha thread waisome comment yako.
 


Unajiona umeongea point saaaaana...Hivi unajua sababu za kaka kutokufanya vizuri madrid
 
Mkuu naunga mkono swala la samatta kuposit picha ambazo azina mahani lifike mwisho cha msingi afanye Kazi kwanza then media zitamfata tena kwa makarmera makubwa cha muhimu hapa akaze buti nahamini hatashida
 
Unajiona umeongea point saaaaana...Hivi unajua sababu za kaka kutokufanya vizuri madrid
Naona unataka mabishano basi ngoja tubishane; relating to hii mada niambie kwanini Kaka hukufanya vizuri Madrid na kwanini CR7, Benzema na Neymar wanafanya vizuri ilhali wauza sura. Keep in mind it should be topic related
 
Lifestyle na picha Ni vitu viwili tofauti. Kuna watu wanapenda picha ila ni very focused, again Cr7, hakuna kocha anayepinga work ethic ya CR7 lakini ni mpenzi wa picha mbaya.

Picha za Samatta karibu zote zinamuonyesha akiwa katika mazingira ya kimichezo which is a good thing tofauti na kama angekua anapiga picha akiwa club au sehemu Zingine za starehe.

Kama mleta uzi anakosoa lifestyle ya samatta basi alete ushahidi zaidi ila kama ni picha tu ambazo zinamuonyesha akiwa michezoni basi hajui alisemalo.
 
Clauds fm wanatafuta kiki ya sports Xtra kupitia kwa mbwana utaskia leo tumezungumza na mbwana hawa jamaaa ndo wanasababisha napicha hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…