Nami nina tamaa hy, ila sijui wachezaji wetu wana nini! Hakuna anayepata timu kwenye ligi kubwa za ulaya, sana sana kwenye ligi zisizo na umaarufu huko vietnam, nk. Tulidhani milango ilifunguka kwa Ngassa kutua EPL badala yake kaishia Azam Fc, na anaonekana kafika, hana hata dalili za kwenda ulaya. Ni changamoto kwa Samatta na vijana wengine wanaochipukia.