Watanzania wengi ni "ma-bogus". Hushindwa kutofautisha masuala(issues) na kuyajadili kwa weledi. NA HUSHINDWA PIA KUELEWA HOJA NA KUELEWA MSINGI WA HOJA HUSIKA.
Ndiyo sababu utaona mtu analeta uzi wenye hoja ya kitaifa kwa faida ya watu wote, lakini "Mapopoma" haraka sana hukimbilia kwenye u-vyama na kuanza kutaja majina ya watu!! KAMA WATU HAWAWEZI KUJUA MATATIZO/MASUALA YA KITAIFA NA KUYAJADILI KWA PAMOJA, HHAKUNA NAMNA YA KUSONGA MBELE! NI MKWAMO.
Rejea mada husika ya Kiingereza cha Mbwana Samatta:
Kiingereza ni lugha tu kama lugha nyingine, haina umaalumu wowote ingawa imetapakaa dunia nzima na ni muhimu sana kuijua.
Kama hukubahatika kusoma na kujifunza Kiingereza, hakuna shida yeyote ukikosea kukiongea au kutokukijua kwasababu si lugha yako.
Lakini kama umesoma hadi Chuo Kikuu, au hadi kidato cha sita na hujui Kiingereza wewe ni mpumbavu tu! Una low IQ, umeshindikana na ni hasara ya mama yako